Maandalizi ya kongamano la kimataifa la Alkafeel awamu ya pili yanaendelea, kamati ya maandalizi yasema kua tafiti zake zina mashiko na zinakidhi viwango vya kimataifa..

Maoni katika picha
Kufuatia maandalizi maalum ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel leo mwezi 12 Shawwal 1438h sawa na 07 Julai 2017m kimefanyika kikao cha kamati ya maandalizi, kilicho hudhuriwa na wajumbe wote wa kamati ya maandalizi kwa ajili ya kujadili mada zitakazo wasilishwa pamoja na malengo yaliyo wekwa na kamati kuu.

Hili linafanyika baada ya mafanikio yaliyo patikana katika awamu iliyo pita, kwa ajili ya kulinda mafanikio hayo yanafanyika maandalizi ya awamu ya pili itakayo fanyika (11-12 Septemba 2017m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Makumbusho ni utamaduni na uchumi) kufuatia maandalizi hayo na kilicho jiri katika kikao hicho; rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Swadiq Laazim alisema kua: “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha makumbusho ya Alkafeel wanafanya maandalizi ya kongamano la pili la kimataifa litakalo kua na maudhui mbalimbali, kumekua na vikao kadhaa katika kipindi huki kwa ajili ya kupendekeza mada muhimu zitakazo wasilishwa katika kongamano zinazo endana na malengo ya kongamano”.

Akaondelea kusema kua: “Tayali mada zitakazo wasilishwa katika kongamano hilo zimesha jadiliwa, nazo zitahusu turathi, uchumi, makumbusho na vitu vingine, kikao hiki kimehudhuriwa na wajumbe wote wa kamati ya maandalizi pamoja na rais wa kamati hiyo, mada zimejadiliwa kwa umakini mkubwa na kuzigawa kwa wajumbe wa kamati”.

Rais wa kamati ya elimu inayo simamia kongamano hili dokta Ibrahim Sarhaan Shimriy amesema kua: “Kamati inayo simamia kongamano la Alkafeel la kimataifa awamu ya pili imejadili tafiti za kielimu zilizo wasilishwa kutoka kwa watafiti na wanachuoni wa turathi, kongamano hili litakua la aina yake kwa kushiriki watafiti kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi (zisizo kua za kiarabu), watafiti walio shiriki ni kutoka: Misri, Ujerumani, Japani, Iran pamoja na Iraq kutoka katika vyuo tofauti”.

Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa makongamano yanayo simamiwa na kuendeshwa na Ataba tukufu, kwa ajili ya kufungua milango ya mawasiliano na kubadilishana uzoefu baina na makumbusho katika ulimwengu wa sasa, katika kongamano hili watashiriki watafiti na watalamu wa mambo ya makumbusho wa ndani na nje ya Iraq.

Kongamano linalenga mambo yafuatayo:

Kwanza: Kulinda urithi wa turathi (vifaa kale) na utamaduni.

Pili: Kusaidia taasisi za kidini kuanzisha makumbusho na kuendeleza elimu ya makumbuso (vifaa kale).

Tatu: Kufungua uwanja wa kusaidiana baina ya taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa.

Nne: Kuongeza heshima za makumbusho kwa kuyapa nafasi maalumu katika vyombo vya habari na kuonyesha umuhimu wake kiuchumi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: