Kituo cha uhuishaji wa turathi chini ya Daru Makhtutwaat katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukaribia kutolewa rasmi kwa idadi kubwa ya jarida la (Khizaanah) katika mtandao wa kielekronik linalo husu turathi kwa mara ya kwanza, miongoni mwa athari kubwa iliyopo katika umma ni urithi wa kifikra unao ambatana na vifaa kale, na nyingi zilizopo sasa ni maktaba kuu na hazina za maktaba.
Hivyo Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza harakati ya kukusanya na kuhakiki turathi hizo na imekua ni fani kamili na kazi inayo jitegemea sawasawa na elimu zingine tofauti.
Ukamilifu wa kazi hiyo; kituo cha uhuishaji wa turathi kimetoa jarida la kielimu linalo elezea vifaa kale na kulipa jina la (Khizaanah), nao ni mradi wa kifikra, lengo kubwa ni kuhuisha elimu na maarifa pamoja na kushajihisha watafiti na watu wanaojua umuhimu wa turathi kuendeleza urithi wao wa kitamaduni, na kuvifanyia ukarabati, kuvihakiki pamoja na kuvichapisha na kuvisambaza kwa ajili ya kunufaika navyo.
Unaweza kuingia katika mtandao kwa anuani hii: http://kh.hrc.iq