Atabatu Abbasiyya tukufu yazipongeza familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi kufuatia kukombolewa kwa mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Hafla zimekua nyingi tena za aina tofauti kufuatia ushindi waliopata wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi watukufu dhidi ya magaidi ya Daesh katika mji wa Mosul na kuurejesha katika serikali ya nchi yetu kipenzi. Atabatu Abbasiyya haijabaki nyuma katika swala hili, imetoa mkono wa pongezi kwa wale ambao walikua sababu ya kupatikana ushindi huu mkubwa, nao ni mashahidi ambao damu zao tukufu ndio zimeleta ushindi huu na kufuta ndoto za Daesh na wafadhili wao.

Kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu, kimetuma ujumbe kwenda kutembelea familia za mashahidi na kuwapongeza pamoja na kuwapa zawadi kufuatia ushindi uliopatikana kwa damu na kujitolea watoto wao watukufu, msafara huo umekwenda sehemu mbili:

Kwanza: Mkoa wa Basra ambako walifanya hafla na kutoa zawadi kwa familia zaidi ya 150 za mashahidi wa Hashdi Sha’bi, kulikua na wazungumzaji tofauti na kaswida za kimashairi, halafu ukafuatia ujumbe wa rais wa msafara; Shekh Swalahu Karbalai ambaye alisema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imebeba jukumu la kutekeleza mradi huu wa kukirimu mashahidi wa familia za Iraq hususan mashahidi wa Hashdi Sha’abi watukufu, mradi huu ulianziswa kutokana na fatwa ya Marjaa dini mkuu, alipo toa fatwa ya kulinda Iraq na maeneo matukufu, bado unaendelea hadi leo”. Akasifu namna walivyo jitolea mashahidi hao, walijitolea namu na nafsi zao, wakafanya mambo mazuri kwa ajili ya kulinda Iraq tukufu, na wakasimama imara kama nguzo dhidi ya magaidi ya Daesh.

Pili: Mkoa wa Dhiqaar; ambako familia 140 za mashahidi zilipatiwa zawadi ukiwemo msaada wa kimanawiyya na kimadiyya pamoja na zawadi kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kikiwemo chakula kutoka katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Shekh mwanajihadi Sultani; ambaye ni mjumbe wa ugeni hio alisema kua: “Hakika lengo la kutoa misaada kwa familia hizi ni kuhakikisha familia za mashahidi na majeruhi zinapata mahitaji muhimu na kutekeleza agizo la Marjaa dini mkuu, ugawaji huo unafanywa kwa kufuata utaratibu maalumu ulio wekwa na kamati inayo simamia utoaji wa zawadi hizo”.

Familia za mashahidi wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kuwazawadia na wakaonyesha kuthamini sana mchango wa kimanawiyya kuliko wa madiyya, na kusema kua umewashajihisha kuendelea kujitolea zaidi kwa ajili ya kukomboa aridhi zote zinazo kaliwa na magaidi ya Daesh.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia maelekezo ya Marjaa dini mkuu hutoa misaada ya lazima kwa familia za mashahidi na majeruhi, na imeandaa utaratibu maalumu wa kutembelea majeruhi na familia za mashahidi katika mikoa yote ya Iraq mfululizo, kwa ajili ya kuwajulia hali na kukidhi mahitaji yao na kuwapa kila aina ya msaada kutokana na kujitolea kwa watoto wao, ziara hizo zinaendelea hadi tuhakikishe tumezifikia familia zote za mashahidi walio fariki baada ya kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: