Muhimu: Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa tamko la kupongeza kukombolewa kwa Mosul na yasisitiza kufaulu kwa fatwa na namna wairaq walivyo ipokea..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya alasiri ya leo Juma Nne (16 Shawwal 1438h sawa na 11 Julai 2017m) imetoa tamko la kupongeza kukombolewa kwa Mosul, tamko hilo limetolewa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Tamko kuhusu ushindi mkubwa wa kukombolewa kwa Mosul kutoka kwa magaidi ya Daesh.

Kutoka katika aridhi ya ushujaa na kujitolea..

Kutoka katika Ataba ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Kutoka katika aridhi takatifu ilipo tolewa fatwa tukufu, ya Marjaa dini mkuu ya kulinda Iraq, raia wake na maeneo matukufu.

Kufuatia kutangazwa kukombolewa kwa mji wa Mosul kipenzi..

Tunawapongeza wale ambao walikua sababu ya kupatikana ushindi huu na kukombolewa kwa miji na vijiji vya Iraq ambapo mji wa mwisho kukombolewa ni Mosul kipenzi..

Tunawapongeza watu hawa watukufu ambao wameshinda mtihani wa Marjaa dini mkuu “Mtu mwenye utukufu wa mwanzo na wa mwisho katika jambo hili”.

Hakika hawa “Wapiganaji shupavu wa vikosi vyote pamoja na tofauti za majina yao, kama vile kikosi cha kupambana na magaidi, wanajeshi wa muungano, vikosi vya jeshi jasiri la Iraq, jeshi la anga, na vikosi vya wapiganaji wa kujitolea, vijana wa makabila ya Iraq, pamoja na familia zao na kila aliye simama pamoja nao na kuwasaidia kwa namna moja au nyingine”. Kama walivyo elezewa na Marjaa mkuu katika hotuba yake.

Tunawapongeza kwa sababu bila wao ushindi usingepatikana.. Wao ni moja ya sababu mbili za ushindi huu.

Wao pamoja na fatwa ndio walio leta ushindi mkubwa dhidi ya magaidi ya Daesh, wamevunja ngome yao (magaidi), na wameiokoa Iraq na miji ya eneo hili na hatari ya ugaidi..

Wao wamepigana kwa niaba ya ubinadamu, wameonyesha ujasiri na ushujaa mkubwa.

Shukrani ziwaendee raia wote wa Iraq, watu ambao Marjaa dini mkuu amewasifu kwa namna ya pekee, akasema kuhusu watu hawa: “Hakika watu wa Iraq wana misingi imara ya ubinadamu na yanayo endelea kwa watoto wao ni kukataa udhalili na uonevu, wamesimama imara kwa hali na mali –hakuna kutu kikubwa zaidi ya damu zao takatifu zinazo mwagika- kwa ajili ya kulinda nchi, heshima na maeneo matukufu, hakika vita hii ya miaka mitatu imethibitisha ushujaa wa wairaq na utayari wao wa hali ya juu kabisa katika kujitolea kwa ajili ya kulinda heshima na utukufu wakati wowote itakapo hitajika, wana wanaume majasiri na wanawake wazalendo wenye uwezo mkubwa wa kupambana na kushinda mitihani inayo sumbua nchi nyingi, ni wajibu wa watu wote kusimama pamoja na kushirikiana ili kuleta ushindi utakao tupa amani na utulivu katika taifa letu Inshallah”.

Hongera yenu wairaq kwa ushindi huu, nawakumbusha tulicho takiwa na Marjaa dini mkuu katika Hotuba yake ya 13 Machi 2015m pale alipo sema: “Ninapenda kusisitiza kwa mara nyingine umuhimu wa kutunza historia hii kwa kuhifadhi kila kitu ili isipotee au kubadilishwa, ni haki ya vizazi vijavyo kuona historia yetu na kuisoma kwa uwazi na uhakika kama sisi tunavyo soma historia ya vizazi vilivyo pita”.

Na kauli ya Muheshimiwa (d.dh.w):

“Amani ya Mmwenyezi Mungu iwe kwenu enyi raia imara wa Iraq wenye subira mmeushangaza ulimwengu kwa subira yenu na ujasiri wenu”.

Mwisho wa maombi yetu tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu na rehema na amani zimuendee mtume Muhammad na watu wake watoharifu.

Tarehe: 16 Shawwal 1438h sawa na 11 Julai 2017m.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: