Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu nyumbani kwa Sayyid Hashim Balushi mmoja wa waheshimiwa wa Karbala..

Maoni katika picha
Sayyid (Haadi Balushi) ni mmoja wa waheshimiwa wa Karbala mwenye historiya ya kuitumikia husseiniyya, mzazi wake alikua mlezi wa moja ya maukibu (kikundi) muhimu kihistoria, ambayo ni maukib ya Azaa Balushi, iliyo anzishwa mwaka (1316h / 1898m), ilianziswa katika mji uliopo kusini ya Karbala tukufu ikijulikana kama (Akdi Balushi).

Wahudumu wa maukibu hii walikua wakihuisha matukio ya kidini majumbani mwao na mitaani, baada ya muda ikawa ni maukibu rasmi inayo shirikiana na maukibu zingine katika kuhuisha siku kumi za kwanza ndani ya mwezi mtukufu wa Muharam.

Maukibu Azaa Balushi hufanya igizo la (kuchomwa mahema) kama sehemu ya kukumbuka kuchomwa mahema ya imamu Hussein (a.s), hutengeneza mahema makubwa na madogo kisha huchomwa hema moja tu, kwa ajili ya kukumbuka kuisha kwa vita.

Hivyo Sayyid Hashim amezaliwa na kulelewa katika mazingira ya kumpenda imamu Hussein (a.s), na hajafanya ajizi katika kuhuisha maombolezo ya mwezi mtukufu wa Muharam na Safar, pia hufanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zahara (a.s) kwa kufanya hafla kubwa tarehe ishirini ya mwezi wa Jamadil-Ula kila mwaka, hafla hizi zimedumu mfululizo kwa miaka zaidi ya 85, Sayyid Hashim anasimamia hafla hizi tangu mwaka 1970m, na alianza kusimamia uhuishaji wa shahada (kufariki) kwa imamu Zainul-Abidina (a.s) tangu mwaka 1960m, pamoja na harakati zingine nyingi ambazo amedumu nazo na hazikusimama hata wakati wa utawala wa Ba’athiy.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha mahusiano imeweka daraja la kuwasiliana na kujenga mapenzi na undugu na watu wote muhimu katika jamii ya Karbala kutokana na wanayo yajua katika turathi na watu muhimu katika kutumikia mwenendo wa imamu Hussein (a.s) katika kipindi cha miaka yote iliyo pita na kuenzi kazi zao tukufu, katika utekelezaji wa jambo hili la kuhuisha mahusiano ya kibinadamu na kiundugu kwa watu ambao majina yao yapo katika historia ya Karbala, ugeni maalumu kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umemtembelea Sayyid (Haadi Balushi) nyumbani kwake, Sayyid ameshukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na viongozi wake kwa heshima kubwa waliyo mpa ya kumtembelea.

Mwishoni mwa ziara hiyo; ugeni ulimpa Sayyid (Haadi Balushi) baadhi ya zawadi kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama sehemu ya kuonyesha kuguswa kwao na utumishi wake kwa imamu Hussein (a.s) na wakamuombea maisha marefu yenye afya tele.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: