Kutokana na mazingira iliyo pitia Iraq na raia wake baada ya kuvamiwa aridhi yake na magaidi ya Darsh, Marjaiyya wameweka plani ya kitaifa itakayo tufusha katika hatua hii, katika plani hiyo kuna nukta muhimu nne ambazo zimefafanuliwa na mwakilishi wa Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai kupitia Hotuba ya pili ya swala ya Ijumaa siku ya (19 Shawwal 1438h sawa na 14 Julai 2017) iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram tukufu ya imamu Hussein (a.s), alibainisha kua:
- 1- Kila mtu atambue kua kutumia nguvu na ubaguzi wa kitabaka na kijamii kama njia ya kupata baadhi ya mambo, haitakua na matokeo mazuru, bali itazidisha umwagikaji wa damu na kuangamiza nchi, na itakua sababu kubwa ya kuingiliwa mambo yetu na watu wengine kitaifa na kimataifa, hakuna upande utakao faidika, wote watapata hasara, na itakua ni hasara ya Iraq nzima – Mola atuepushe na hilo-.
- 2- Waliopo katika nafasi za utendaji serikalini wafanye kazi wakijua kua; raia wote pamoja na tofauti zao za kijamii, kidini na kimadhehebu wako sawa katika haki za msingi, hakuna ubora wa mmoja kwa mwingine ispokua kwa utekelezaji wa sheria. Msingi huu ukifatwa kwa ukamilifu utasaidia kutatua matatizo mengi na kurejesha uaminifu kwa serikali na taasisi zake, hakika ni muhimu kupambana na ufisadi wa kiofisi na kimali pamoja na kujitenga na maslahi binafsi, ya kikundi au chama.
- 3- Kuachana na maslahi ya vyama (uchama) na kuzingatia uwezo wa mtu na uadilifu wake katika uteuzi wa nafasi za uongozi wa taifa, hakuna nafasi ya kujinasua katika matatizo ikiwa ufisadi na utabaka vitaendelea katika ofisi za serikali.
- 4- Hakika kuwatunza majeruhi na watu wenye matatizo pamoja na familia za mashahidi na kuwafanya waishi maisha ya kawaida ni jambo la wajibu kwa wote, na ni wajibu zaidi kwa serikali na wabunge, sio sahihi kutowapa mahitaji yao kwa kisingizio cha uchache wa mali, hakika serikali inamaeneo mengi inaweza kubana matumizi na kuwapa watu hawa, kimesha pangwa kiwango kidogo cha mshahara watakao kua wakipewa watu hawa kwa ajili ya kuwapunguzia ukali wa maisha, muogopeni Mwenyezi Mungu na tambueni mtaulizwa kuhusu wao.