Umoja wa taasisi za malezi wazizawadia shule mbili za msingi za Ameed kwa kupata ufaulu wa asilimia %100..

Maoni katika picha
Umoja wa taasisi za malezi zisizo kua za kiserikali zimetoa zawadi kwa shule mbili za msingi za Ameed zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kupata ufaulu wa asilimia %100, pamoja na kumzawadia mwanafunzi Mina Haidari, mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Ameed kwa kua mwanafunzi wa kwanza katika mkoa wa Karbala kwa ufaulu wa asilimia %100.

Zawadi hizo zilitolewa katika hafla iliyo simamiwa na mkuu wa malezi wa mkoa wa Karbala, wanafunzi walio faulu vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi ya mwaka (2016-2017m) walipewa zawadi hizo mbele ya rais wa kamati ya uongozi wa mkoa mtukufu wa Karbala pamoja na baadhi ya wabunge wa Iraq na wawakilishi wa shule ya msingi ya Ameed ya wavulana na wasichana.

Hafla ilipambwa na nasaha kutoka kwa watu tofauti, akiwemo rais wa kamati ya uongozi wa mkoa wa Karbala ambaye alisema kua: “Hakika ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, leo hii unaenziwa kwa elimu, maarifa na ujenzi wa taifa, nao ni ushindi wa raia, umma na misingi ya itikadi sahihi, haya yote yamepatikana kutokana na fatwa tukufu ya Marjaa dini mkuu, hakika huu ushindi mkubwa wa kihistoria dhidi ya genge la magaidi la Daesh, lazima uenziwe na ushindi wa elimu maarifa na ujenzi wa taifa, na Karbala tukufu ndio chemchem ya ushindi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: