Sayyid Swafi asifu umahiri na uwezo wa madaktari wa ki-iraq na amewaomba kujiendeleza zaidi wafikie kiwango cha ubora wa nchi zilizo endelea..

Maoni katika picha
Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmad Swafi (d.i) amewasifu madaktari wa ki-iraq na kuwataka waiache kujiendeleza, ili kuboresha sekta hiyo na huduma zinazo tolewa kwa wananchi.

Hayo aliyasema katika kikao alicho fanya na madaktari wa mkoa wa Karbala ndani ya hospitali ya rufaa Alkafeel mbele ya kiongozi mkuu wa hospitali hiyo daktari Haidari Bahadeli, walijadiliana mambo mbalimbali katika kikao hicho, yanayo husu sekta ya afya nchi Iraq kwa ujumla na yanayo husu mji mtukufu wa Karbala, Sayyid Swafi alizungumza mambo mengi miongoni mwa mambo hayo ni:

  • 1- Kuhakikisha vinapatikana vifaa tiba vya kisasa ili kuboresha sekta ya utabibu nchini Iraq.
  • 2- Kuboresha huduma za matibabu kwa raia wa Iraq.
  • 3- Kuongeza uwezo wa madaktari wa Iraq na kuboresha mazingira ya kazi.
  • 4- Kunufaika na madaktari wa kigeni wanaokuja katika hospitali za hapa nchini ikiwemo hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo imesha fungua milango hiyo.
  • 5- Kuna mafanikio yaliyo fikiwa na madaktari wa Iraq yanashinda yale yanayofikiwa na madaktari wa kigeni, mafanikio hayo yanapasa kuenziwa.
  • 6- Kuangalia uwezo wa wauguzi na kuendeleza vipawa vyao na uwezo wao.
  • 7- Umuhimu wa kuwepo na jopo la madaktari bora wa Iraq na kusaidia kufanya majukumu yao.
  • 8- Kukamilisha mahitaji yote muhimu katika kuongeza uwezo wa madaktari na kuwafanya wafikie kiwango kikubwa cha udaktari sawa na wale waliopo katika dunia ya kwanza.
  • 9- Kuweka mbele ubinadamu katika utoaji wa huduma za kidaktari.

Mwisho wa kikao hicho muwakilishi wa madaktari wa Karbala alisifu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel kwa wakazi wa Karbala tangu ilipo funguliwa hadi sasa, na akaomba ishee uzoefu wake na taasisi za afya za serikali, ikiwa ni pamoja na kuagiza madaktari bingwa watakao kuja kufanya kazi pamoja na madaktari wa Iraq ili kuongeza uwezo wao na kuwapa uzoefu zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: