Kujiandaa na mitihani yao: Wanafunzi wanaojiandaa na mitihani wakimbilia Atabatu Abbasiyya kwenda kujisomea, nayo yawaandalia mazingira mazuri..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kila siku inapokea makumi ya wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya upili (sekondari) iliyo anza mwezi huu ambao hali ya hewa imefika zaidi ya nyuzi joto 50, pamoja na kuwepo kwa tatizo la kukatika katika kwa umeme, pia kuna msukumo wa kinafsi unao wafanya wapate utulivu na amani wanapo kua wakijisomea masomo yao wakiwa jirani na kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), wanafunzi wengi hupenda kujisomea ndani ya Ataba tukufu wale wanao ishi maeneo ya karibu na haram hata wale wanao ishi mbali; nje ya mji wa Karbala.

Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafunzi wameandaliwa sehemu nyingi za kujisomea mmoja mmoja au kwa kikundi, kuna wanaokaa katika eneo la chini (sardabu) na wengine wakikaa katika korido za haram tukufu huku wengine wakisomea ndani ya maktaba ya Ataba tukufu na wengine wakikaa katika uwanja wa haram, wana uhuru wa kuhama hama ndani ya maeneo hayo, mambo muhimu yote yanayo hitajika yapo, kama vile maji ya baridi, taa na kiyoyozi (a/c) kwa kuwepo vitu hivyo pamekua ni sehemu nzuri zaidi ya kujisomea.

Wanafunzi wamebainisha kua; mazingira ya Ataba tukufu yanatofautiana sana na mazingira ya nyumbani au katika viwanja na bustani za umma ambako baadhi ya wanafunzi huenda kujisomea sehemu hizo, hii yote inatokana na maandalizi mazuri yaliyo fanywa na Ataba tukufu kwa ajili ya mazuwaru na wanafunzi, hakika mazingira hayo yanamsaidia mwanafunzi kuzingatia na kuhifadhi masomo yake hususan anapo kua anajiandaa kwa ajili ya mitihani ya mwisho, hali kadhalika mazingira haya yanatupa nguvu tuwapo karibu na Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kuchukua ahadi kwake ya kufanya vizuri na kufaulu katika mitihani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: