Miongoni mwa ratiba zake za kusaidia wakimbizi, kamati ya misaada chini ya ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh), imepeleka shehena ya misaada ya tani za vyakula kwa watu waliokimbia hivi karibuni katika vita ya kukomboa mji wa Mosul, kwa ajili ya kupunguza ukali wa maisha wanayo pitia kwa sasa hususan wazee na watoto, kamati hii imekua ikitoa misaada ya kibinadamu kila wakati.
Rais wa kamati ya misaada Sayyid Shaheed Mussawiy alisema kua: “Baada ya kupata habari kuhusu hali ngumu waliyo nayo wakimbizi wa upande wa kulia wa mji wa Mosul, na hasa wale walio kua wanakaa katika kitongoji cha Mosul ya zamani, kamati ya misaada imebeba shehena kubwa ya vyakula na kuziletea familia hizi zilizo fanya makazi yao kua katika vitongoji vya Twairani, Hawiy, Jusiq, Dundani, Jawiq na sehemu zingine, pamoja na joto kali na ubovu wa barabara zinazo elekea maeneo hayo, pamoja na upande wa kulia wa mji wa Mosul, tumeweza kufikisha misaada na kusimama pamoja nao katika mazingira magumu kutokana na msaada wa wanajeshi wa umoja”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika tumegawa tani (18) za unga na tani (25) zilizo jumuisha aina tofauti za nafaka na kuwekwa katika vikapu (2500) hali kadhalika tumegawa katon (2500) za maji, vile vile tumegawa maji katika hema la marjaiyya lililopo katika kata ya Hamaam Aliil”.
Sayyid Shaheed akaendelea kubainisha kua: “Kamati ilipokelewa kwa maneno mazuri ya ukaribisho yaliyo jaa sifa na shukrani kwa Muheshimiwa Marjaa dini mkuu kutoka kwa tabaka zote za raia wa Iraq, na baada ya kumaliza kugawa misaada hiyo, familia za wakimbizi walitoa shukrani kubwa kutokana na upendo wa hali ya juu kabisa kutoka kwa Marjaa dini mkuu na wakawaagiza wajumbe wa kamati hii wafikishe salamu na dua zao kwa Muheshimiwa Marjaa dini mkuu”.
Kumbuka kua misafara ya kusaidia inaendelea kama ilivyo pangwa katika hema za wakimbizi na katika miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kuwapunguzia ukali wa maisha, na kuwafanya watambue kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wananchi wote wa Iraq, na kuondoa picha hasi inayo wekwa na maadui.