Muendelezo wa ratiba za wanawake, Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeendeleza ratiba ya masomo ya msimu wa joto (kiangazi) ambapo hua ni kipindi cha likizo za kiangazi, husomeshwa masomo ya Qur’an tukufu pamoja na masomo mengine kwa lengo la kutoa malezi mema kwa wasichana yanayo endana na mafundisho ya Qur’an pamoja na tabia na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watoharifu (a.s).
Selibasi ya masomo imeandaliwa na wasomi walio bobea katika fani za Qur’an; usomaji, hukumu na hifdhu pamoja na masomo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaq. Masomoa yote yanafundishwa kulingana na umri na viwango vya washiriki, hali kadhalika wanafundishwa kazi za mikono kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.
Semina hizi zinaendeshwa katika tawi la Maahadi mjini Najafu, Atabatu Abbasiyya imeandaa nyaraka zote muhimu za kusomea pamoja na usafiri, semina imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanawake, kutokana na ukweli kua; hii ni fursa muhimu kwao ya kuongeza kiwango cha elimu na kunufaika na kipindi hiki cha likizo.