Kamanda wa kikosi cha umoja Raaid Shaakir Judat amesema kua; misaada iliyotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu imechangia sana katika kujenga ari ya wapiganaji walio kua wakitimua vumbi dhidi ya magaidi ya Daesh, pamoja na usia wa kiongozi wa kisehia Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.dh).
Aliyasema hayo akiwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) katika hospitali ya rufaa Alkafeel, baada ya kupewa pongezi na muheshimiwa huyo kufuatia ushindi mkubwa walio pata wa kuwatimua magaidi ya Daesh katika mkoa wa Mosul na kuurejesha katika himaya ya taifa, na akawarehemu mashahidi waliojitolea roho zao katika ukombozi wa mji huo, na akamuomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka majeruhi na kuwapa afya njema, hali kadhalika Sayyid Swafi alisifu ushujaa wa jeshi la umoja katika vita kali waliyo endesha pamoja na vikosi vingine.
Mwisho wa kikao hicho kamanda Raaid Shaakir Judat; alitoa shukrani nyingi kwaniaba ya wapiganaji wa jeshi la umoja kwa Muheshimiwa Sayyid Swafi kutokana na misaada mingi wanayo toa kwa wapiganaji hao katika uwanja wa vita vya kukomboa miji iliyo kua chini ya udhibiti wa magaidi ya Daesh.
Pia kamanda (Judat) aliwapa midani ya jeshi la umoja viongozi wa hospitali ya Alkafeel iliyo pokelewa na mkuu wa hospitali hiyo dokta Haidari Bahadeli, kutokana na msaada wao mkubwa katika kuwatibu wapiganaji wanaopata majeraha vitani, huduma hiyo ni muhimu sana katika kufanikisha ushindi na kukomboa miji iliyokua chini ya magaidi.
Kisha kamanda Judat akatembelea majeruhi wa jeshi la umoja walio lazwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, na akajionea huduma nzuri za kimatibabu wanazo pewa.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel ni kiigizo chema kwa taasisi zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu, toka kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda imechukua jukumu la kusaidia kuwatibu majeruhi na inafanya kila iwezalo kupunguza machungu yao, haya yote inayafanya kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo himiza kufanya hivyo kama sehemu ya wajibu wake kwa majeruhi.