Wizara ya malezi yaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa himaya wanafunzi na kuwasaidia katika siku wanazo jiandaa kwa ajili ya mitihani na yasisitiza kua kwa kufanya hivyo inasaidia sekta ya malezi na elimu ya Iraq..

Maoni katika picha
Wizara ya malezi imeonyesha umuhimu wa kitendo cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kuwafungulia milango wanafunzi wanao jiandaa na mitihani, na kuwawekea mazingira mazuri ya kujisomea kutoka kuanza kwa mitihani ya mwisho ya wanafunzi wa shule za upili (sekondari, O levo na A levo).

Ofisi ya habari ya waziri dokta Muhammad Iqbaal imesema kua; Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu kuandaa mazingira bora ya kujisomea kuna umuhimu mkubwa sana hususan katika kipindi hiki cha joto kali na matatizo ya umeme, wakasisitiza kua jambo hilo linachangia pakubwa sekta ya malezi na elimu hapa Iraq.

Wakaashiria kua, mambo kama haya hua na nafasi maalumu pia yana athari nzuri kwa wananchi.

Kumbuka kua; kutokana na maelekezo ya viongozi wakuu, Atabatu Abbasiyya tukufu, imewaandalia wanafunzi sehemu nyingi za kujisomea mmoja mmoja au kwa kikundi, kuna wanaokaa katika eneo la chini (sardabu) na wengine wakikaa katika korido za haram tukufu, huku wengine wakisomea ndani ya maktaba ya Ataba tukufu, na wengine wakikaa katika uwanja wa haram, wana uhuru wa kuhama hama ndani ya maeneo hayo, mambo muhimu yote yanayo hitajika yapo, kama vile maji ya baridi, taa na kiyoyozi (a/c) kwa kuwepo vitu hivyo pamekua ni sehemu nzuri zaidi ya kujisomea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: