Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuawa kishahidi kwa chemchem ya elimu na utamaduni wa uislamu Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) baada ya adhuhuri ya Alkhamisi ya leo (25 Shawwal 1438h) sawa na (20/07/2017m), kundi la waombolezaji ambao ni watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) lilifanya matembezi kuanzia Atabatu Abbasiyya na kuelekea katika malalo ya imamu Hussein (a.s), huku wakiwa na huzuni kubwa, walienda hadi katika uwanja wa haram ya Sayyid Shuhadaa (a.s).
Walihuisha kumbukumbu ya msiba huu kwa kufanya majlisi ya maombolezo na kusoma ziara pamoja na kufanya ibada zingine ndani ya uwanja wa haram tukufu ya imamu Hussein (a.s) na kutoa mkono wa pole kwa imamu wa zama (a.f).
Kufuatia msiba huu kuta za Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) zimewekwa mapambo meusi na kufungwa taa nyekundu kwa ajili ya kuonyesha ukubwa wa msiba huu.