Kukamilika kwa hatua ya kwanza ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa..

Maoni katika picha
Kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur’an tukufu chini ya Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika kwa hatua ya kwanza ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, iliyo anza katika mwezi huu wa saba na kushiriki idadi kubwa ya wataalamu wa Qur’an kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, baada ya kutimiza masharti yaliyo wekwa na kamati na kukubaliwa kushiriki muda mfupi kabla ya kuanza kwake.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa mradi huu Ustadh Ali Bayati “Hatua hii ilidumu siku kumi, washiriki walisoma mambo mbalimbali ya kitamaduni na kimalezi, yanayo lenga kuwaandaa washiriki na kuwawezesha kua na kiwango kizuri katika masomo ya Qur’an, katika awamu hii wamesomeshwa mahadhi ya usomaji ya aina nne, (Mahadhi ya Hafidh Khaliil Ismail, Shekh Muhamma Swidiq Minshawiy, Shekh Abdulbasit Muhammad Abdu Swamad na Shekh Shahata Muhammad Anwar) chini ya wakufunzi sita (6) mahiri wa mahadhi hizo”.

Akaongeza kusema kua: “Awamu zijazo zitashuhudia maendeleo makubwa hususan kwa wale wanaofuta maelekezo ya walimu wao walio wasimamia katika mafundisho haya ya kuongeza maarifa”.

Kumbuka kua mradi huu ni miongoni mwa miradi mingi inayo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu, unalenga kutengeneza kizazi cha wasomi wa Qur’an tukufu, hususan watoto wenye vipaji vya usomaji, kwa kuwapa semina za muda mfupi, mradi huu unalenga wanafunzi wa shule za msingi na za upili (sekondari) kutoka katika mikoa tofauti ya Iraq, pia mradi huu unakusudia kunufaika na muda wa likizo za kiangazi kwa kuandaa kundi kubwa la wasomaji wa Qur’an na kuhakikisha wanafikia kiwango kizuri katika usomaji wa Qur’an, katika kipindi cha miezi miwili takriban katika sehemu ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: