Idara ya umwagiliaji chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutengeneza bebeo za kuhifadhia dum za maji ya kuziweka katika maeneo ya karibu na uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika baadhi ya njia zinazo elekea katika haram, kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea msimu wa joto kali la kiangazi, kazi hii inafanywa kwa kushirikiana na kitengo cha uhandisi cha Ataba tukufu.
Mkuu wa idara hii Haji Ahmad Hanun alielezea kuhusu mradi huu, akasema: “Tulipata fikra ya kutengeneza bebeo hizi baada ya kuona njia ya zamani sio rafiki na inafaida chache, jambo la pili tenki za zamani mbaka ufungue kwa mkono wakati wa kunywa maji njia ambayo sio ya kijamii zaidi, ndipo tukaona kuanzisha utaratibu huu wa kuweka bebeo hizi.
Akaongeza kusema kua: “Kila bebeo moja lina dumu nne za maji jenye ujazo wa lita 40 zimekaa kwa urefu na kufunikwa vizuri, zinafunguliwa na mtu maalumu anaye simamia bebeo hilo kwa mkono, dumu hizo zimefungwa vizuri haziwezi kufunguliwa na mtu mwingine, pembeni ya bebeo kuna tenki la maji ya baridi la lita 1000 kwa ajili ya kujaza maji katika dumu hizo yanapo isha au kupungua.
Akaendelea kusema kua: “Kutokana na utaratibu tulio taja, tumeandaa gari zinazo jaza maji katika tenki hizo, gari hizo hupita kwa shida katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi, kwa sasa kazi ya kuweka maji inafanyika kwa urahisi, tumesambaza matenki haya kama hatua ya kwanza, hatua zijazo tutaweka mifuniko maalumu itakayo wawezesha mazuwaru kunywa maji kwa urahisi”.