Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea kufungua milango ya kusaidiana na kushirikiana na taasisi pamoja na vituo vya kiutafiti katika mji mtukufu wa Qum..

Maoni katika picha
Ugeni kutoka kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetembelea taasisi na vituo vya utafiti pamoja na watu muhimu katika dini huko Qum, kwa lengo la kuendelea na mpango wake wa kujengo uhusiano na taasisi pamoja na vituo vya utafiti vya kimataifa, na kubadilisha mawazo sambamba ya kufungua milango ya kusaidiana na kushirikiana.

Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaongozwa na rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu Shekh Ammaar Alhilaliy, kafuatana na wawakilishi wa vituo vya turathi vya Karbala, Hilla, na Basra vilivyo chini ya kitengo hicho, wamefanya vikao vingi na viongozi wa vituo vya utafiti na kujadiliana nao kuhusu uhakiki wa vifaa kale na kubadilishana uzowefu katika sekta hiyo, ugeni ulipata nafasi ya kuangalia uhakiki wa mwisho uliofanywa kwa mafanikio na wahakiki hao, pia waliwatembelea watu muhimu, taasisi na vituo vya uhakiki katika mji wa Qum na wakaangalia mradi maalumu wa kuhakiki vifaa kale vya mji wa Karbala, Hilla na Basra.

Taasisi, watu binafsi na vituo vya utafiti, wote walionyesha utayari wao wa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa jambo lolote wanalo hitaji, ikiwa ni pamoja na kufanya makongamano na nadwa za kitafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: