Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza uzinduzi wa nyumba za makazi za Abbasi (a.s) kua utafanyika mwanzoni mwa mwezi wa Nane mwaka huu 2017m, baada ya kukamilisha mambo yote ya msingi katika nyumba hizo, uzinduzi huo utafanyika katika moja ya bustani zake kubwa, itatumika kura katika ugawaji wa nyumba hizo zipatazo 831 kwa wanufaika.
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh alimesema kua: “Hivi sasa yanafanyika maandalizi ya kuzindua moja ya miradi mikubwa iliyokamilishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ni mafanikio makubwa yaliyo fikiwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), bila kusahau juhudi za watumishi wa kitengo cha uhandisi hususan walio simamia mradi huu na shirika ambao ndio watendaji wakuu tutokana na utalamu wao tumefanikisha mradi huu, ambao umekua gumzo katika mkoa wa Karbala, kwani haujawahi kutokea mradi wa nyumba za makazi mkubwa kama huu tena kwa wasifu na ukamilifu wa viwango vya juu kiasi hiki”.
Mkuu wa shirika lililo tekeleza mradi huu (Shirika la Sibtwain la ujenzi) Ustadh Maahir Abdul-ameer Salmaan alisema kua: “Pamoja na mazingira magumu ya pesa kipindi cha utekelezaji wa mradi huu, lakini kutokana na msaada wa karibu wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu na maelekezo ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) tulifanikiwa kuishinda mitihani hiyo na kukamilisha mradi huu kwa ufanisi kama ulivyo pangwa”.
Akasisitiza kua: “Hakika kazi zote zilizo fanywa katika mradi huu zimehakikiwa kwa umakini mkubwa na wasimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi, na sisi kama shirika tulio tekeleza mradi huu tunaona wazi mazingira magumu ya upatikanaji wa pesa katika nchi yetu ya Iraq hali kadhalika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo hili haikua sababu ya kukwama kwa mradi tuliendelea na ujenzi tena kwa kiwango kilekile tulicho kubaliana bila kupungua hata kidogo”.
Fahamu kua lengo la mradi huu ni kuonyesha thamani ya juhudi zinazo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuwapatia nyumba bora za makazi zinazo endana na maendeleo ya ulimwengu wa kisasa, watapewa nyumba hizo kwa bei ya punguzo.
Kumbuka kua mradi huu umejengwa katika eneo lenye ukubwa wa dunam 122 (305000 mt) na kuna nyumba za ghorofa 831 pia kuna nyumba za chini, kituo cha afya, nyumba za wahudumu na shule, katika eneo la baina ya Najafu na Baabil, sehemu ya makutano ya barabara ya Karbala – Baabil na Karbala – Najafu.