Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu wahudhuria ufunguzi wa maonyesho ya bendera yanayo endeshwa na chuo kikuu cha Kufa..

Maoni katika picha
Kufuatia ushindi mkubwa wa wapiganaji wetu mashujaa, jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi katika aridhi ya Mosul na kwa uhudhuriaji wa ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, siku ya Juma Mosi ya (27 Shawwal 1438h) sawa na (22 Julai 2017m) chuo kikuu cha Kufa kimezindua maonyesho ya bendera katika uwanja wa chuo yenye kauli mbiu isemayo (Bendera na alama za Iraq za zama na zama) chini ya ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari.

Maonyesho hayo yalipata mahudhurio makubwa ya viongozi wa kidini na kisiasa, yalikua na aina mbalimbali za bendera; bendera za jamii za watu wa zamani wa Ashuriyya na Babelon, pamoja na bendera za manabii na maimamu na bendera za kiislamu, zikiwepo bendera maalumu za watu walio tawala katika nchi ya Iraq toka kuasisiwa kwa taifa hili hadi sasa, hali kadhalika kilikuwepo kitengo kilicho onyesha zana zilizo tumiwa na magaidi katika kuadhibu wananchi wema.

Rais wa chuo cha Kufa aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunatoa mkono wa pongezi kwa walimwengu wote kufuatia ushindi walio pata wapiganaji wetu mashujaa dhidi ya magaigi ya Daesh, kutokana na ushindi huo tumeamua kufanya maonyesho haya ya bendera za Iraq, maonyesho ambayo yamehusisha bendera tofauti, zikiwemo za kiislamu na za kijamii pamoja na picha za viongozi na wafalme walio tawala Iraq, pamoja na picha iliyo onyesha ramani ya Iraq kaskazini na kusini, kwa hakika hatuwezi kusahau umuhimu na nafasi kubwa ya Ataba tukufu katika ushindi huu tunao ushuhudia leo, hususan Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ilikua na mchango mkubwa sana katika kutoa misaada ya hali na mali kwa wapiganaji watukufu, na kuwatembelea mara kwa mara katika viwanja vya vita, toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya jihadi hadi leo, pamoja na kuwasimamia wakimbizi na kuwasaidia, kama mnavyo ona hata leo Ataba tukufu imetupa bendera za thamani kubwa; bendera za maimamu ili nazo zishiriki katika maonyesho haya, tunatoa shukrani za dhati kwa viongozi wa Ataba”.

Waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu dokta Abdurazaaq Issa akasema kua: “Leo hii tumeshuhudia maonyesho haya matukufu ambayo yametunza historia ya Iraq na itakua ni kumbu kumbu kwa vizazi vijavyo, vijana wengi wa leo hawatambui historia hii, maonyesho haya yana nafasi kubwa sana ya kukumbusha historia tukufu, hii ni hatua nzuri sana yapasa kuwashukuru walio andaa maonyesho haya, kuhusu ushindi mkubwa uliopatikana katika mji wa Mosul natoa pongezi kubwa kwa raia wa Iraq, hakika yapasa kumpongeza na kumshukuru kila aliye changia ushindi huu dhidi ya magaidi ya Daesh, bila kumsahau Marjaa dini mkuu yeye ndiye sababu ya ushindi na amani ya Iraq, vilevile shukrani za pekee kabisa ziwaendee walio itikia wito wa fatwa tukufu ambayo imepelekea kukombolewa kwa aridhi ya Iraq kutoka mikononi mwa magenge ya kigaidi na kitakfiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: