Bado Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Landan inaendelea kufanya semina mbalimbali za Qur’an, pamoja na kutoa mihadhara na nadwa kuhusu Qur’an tukufu inayo lenga kujenga jamii ya kiislamu yenye kufuata misingi ya Qur’an na kuinua kiwango cha uwelewa wa Qur’an kwa watu wa rika zote, semina iliyo fanyika kwa kushirikiana na jumuiya ya Ahlulbait (a.s) katika mji wa Scotlend na ile iliyo malizika hivi karibuni katika mji wa Jilasco Scotlend ni sehemu tu ya mfululizo wa semina hizo.
Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla hii na msimamizi mkuu wa semina hizi Shekh Dhiyaau Dini Aali Majid Zubaidiy mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha ametuambia kuhusu semina hizi kua: “Semina hizi ni sehemu ya semina zinazo fanywa na tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu la Uingereza ambalo linajitahidi kufikisha elimu ya Qur’an kwa waislamu, na zinapata ushiriki mkubwa kutoka kwa walimu wa Quran na wadao wengine wa Qur’an tukufu”.
Akaongeza kusema kua: “Hafla ya kuhitimisha semina ilihudhuriwa na mkuu wa tawi la Maahadi la Landan Ustadh Muhammad Mudhafar na mkuu wa Jumuiya ya Ahlulbait ya Scotlend Ustadh Izaam Muhammad Yusufu, ambaye katika ujumbe wake aliishukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuendesha semina hii, na juhudi kubwa zinazo fanywa na Maahadi katika kufundisha Qur’an, na akapongeza juhudi hizo”.
Mwisho wa hafla hii vyeti vya ushiriki viligawiwa kwa wanasemina vikiwa na muhuri wa Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya pamoja na kuwapa walimu na wasimamizi vyeti vya kuwashukuru.