Bibi Maasuma alizaliwa mwezi mosi Dhulqa’dah mwaka 173h katika mji wa Madina, alilelewa chini ya uangalizi wa ndugu yake imamu Ridha (a.s), kwa sababu kiongozi wa bani Abbasi Haruna; alimuweka gerezani baba yake imamu Mussa bun Jafari (a.s) mwaka alio zaliwa, kisha akamuua kwa sumu katika mwaka wa 183h, hivyo akaishi chini ya uangalizi wa kaka yake imamu Ridha (a.s).
Imepokewa kua kaka yake imamu Ridha (a.s) ndiye aliye mpa jina la “Maasuma” kama ilivyo pokewa kua babu yake imamu Swadiq (a.s) alimpa jina la “Karima Ahlulbait” kabla hajazaliwa na mama yake bibi Tuktam. Bibi Maasuma kaburi lake lipo katika mji mtukufu wa Qum, limejengewa kubba kubwa na pana uwanja mkubwa, kuna watumishi na wakfu nyingi, nalo ni tulizo la macho la watu wa Qum, watu kutoka sehemu mbalimbali na hufunga safari na kwenda kumzuru (a.s) kila mwaka.
Kuna riwaya nyingi zinazo elezea utukufu wa kumzuru bibi Fatuma (a.s) miongoni mwa riwaya hizo ni:
- 1- Kutoka kwa Sa’adi bun Said, kutoka kwa Abu Hassan Ridha (a.s) anasema: Niliuliza kuhusu kaburi la Fatuma bint Mussa bun Jafari (a.s) akasema: Atakaye mtembelea atapata pepo.
- 2- Imamu Jawaad anasema: Atakae tembelea kaburi la shangazi yangu huko Qum atapata pepo.
- 3- Kutoka kwa Sa’adi, kutoka kwa imamu Ridha (a.s) alisema: (Ewe Sa’adi, mnakaburi letu) nikasema.. kaburi la Fatuma bint Mussa? Akasema, ndio. Atakae lizuru huku anatambua haki yake atapata pepo.
- 4- Imamu Swadiq (a.s) anasema: Hakika Mwenyezi Mungu ana haram ambayo ni Makka, na Mtume (s.a.w.w) anaharam ambayo ni Madina, na Kiongozi wa waumini (a.s) anaharam ambayo ni Kufa, na sisi tuna haram katika mji wa Qum, atazikwa katika mji huo binti miongoni mwa kizazi changu aitwae Fatuma, atakae mzuru atapata pepo.
Mmoja wa washairi anasema kua:
Ewe binti Mussa mtoto wa watakasifu dada wa Ridha na kipenzi wa Jabbaar.
Ewe lulu wa bahari ya elimu umedhihirika kwa Mwenyezi Mungu utukufu wako.
Wewe ni tunu ya Imamu mtukufu fahari ya ukarimu na mwenye siri.
Ewe binti wa uongofu umeendelea kua mtakasifu kwa kila jambo lisilo mfurahisha Mola.
Atakae zuru kaburi lako malipo yake ni pepo hivi ndivyo imepokewa katika riwaya.