Siku ya jana Juma Nne (1 Dhulqa’adah 1438h sawa na 25 Julai 2017m) ilianza semina yenye anuani isemayo: (Vipi tunazifanyia kazi riwaya za Ahlulbait –a.s-) inayo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Landan chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Semina hii inamihadhara sita inayo sherehesha na kufafanua mambo yanayo husiana na riwaya za Ahlulbait watakasifu – wanye nafasi sawa na Qur’an tukufu- na namna ya kuzitambua riwaya zilizo pokelewa kwa njia sahihi na zenye uzito, na mambo yaliyo tegemewa na kufatwa na wanachuoni wengine katika zama zote, na kufahamu sanadi na matini na yaliyopo ndani ya Qur’an na kwa kizazi kitakasifu.
Mkufunzi wa semina hii ni mkuu wa kituoa cha Maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Dhiyaau Dini Aali Maajid Zubaidiy.
Pia semina hii inarushwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii Skype na Face book na kupata ushiriki mkubwa kutoka kwa watu wa Holand, Skotlend na miji mingine ya Uingereza.
Washiriki wa semina hii watatunukiwa vyeti kutoka katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya katika hafla ya kufunga semina.