Uongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji wawaita wapiganaji 3000 wa hakiba..

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji wawaita wapiganaji wake 3000 kwa ajili ya kujiandaa na vita ya kukomboa mji wa Tal-afar.

Hii ni kwa mujibu wa tangazo la uongozi, na wakufunzi wa Abbasi (a.s) wa kivita watashiriki katika kuwaandaa wapiganaji, na kuwaandalia zana za lazima kwao, watakua na muda wa siku saba tu za kuwachuja wapiganaji na kuchagua wale ambao wanastahili kuingia vitani.

Uongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) umefurahi sana kuchaguliwa kua miongoni mwa vikosi rasmi vitakavyo pigana katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, lakini furaha yao ingekua kubwa zaidi kama vikosi vyote vya Hashdi Sha’abi vingeshiriki katika vita hiyo muhimu, wakati huohuo yatupasa kukumbuka usia wa Marjaa dini mkuu unaowataka wapiganaji waendelee kua na moyo wa kupigana kwa ari kubwa kama walivyo na wajihadhari sana kupuuza au kuzembea madamu bado kuna sehemu ya aridhi iko katika udhibiti wa magaidi ya Daesh.

Kumbuka kua kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kimepewa taarifa rasmi na viongozi wakuu wa jeshi ya kushiriki katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: