Maahadi ya Wataalamu wa Alkafeel na uendelezaji wa vipaji wameanzisha program ya mauzo ya mtandaoni..

Moja ya sehemu za Program
Miongoni mwa mfululizo wa matoleo yake ya Program za utoaji wa huduma za kimtandao, Maahadi ya Wataalamu wa Alkafeel na uendelezaji wa vipaji chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanzisha program ya mtandaoni iitwayo (Alwasiit) inayo simamia mambo ya kununua na kuuza katika mtandao, imesanifiwa na kupangiliwa na wataalamu wa Maahadi kwa mujibu wa mahitaji ya soko la Iraq.

Mkuu wa Maahadi hii Ustadh Samir Swafi ametuelezea vipengele muhimu katika program hii akasema: “Program ya Wasiit inavitu vingi vinavyo ifanya ionekane bora kushinda zingine zilizopo hivi sasa, nitataja baadhi ya vitu vilivyopo katika program hii vinavyo endana na soko la Iraq, navyo ni kama vifuatavyo:

  • 1- Kurahisisha uandishi wa mkataba wa mauzo, hususan aridhi, nyumba na magari.
  • 2- Kuna program maalum ya vielelezo vya muuzaji au mnunuzi.
  • 3- Kuna taarifa mbalimbali za vielelezo vya uuzaji au ununuzi pamoja na taarifa za aridhi na nyumba.
  • 4- Inamrahisishia mtumishi wa ofisini kupata taarifa za fedha za ndani na za kigeni.
  • 5- Program hii inaweza kutumiwa na ofisi za uuzaji wa viwanja, madalali na wauzaji wa magari.
  • 6- Wepesi wa utumiaji wa program, inavitu vingi na vinaonekana kwa urahisi.
  • 7- Uwezekano wa kutuma na kupokea mafail.
  • 8- Uwezekano wa kuchukua nakala ya hakiba na kuirejesha wakati wowote ukitaka.
  • 9- Uwezekano wa kupakua na kurudufu (kuprinti) ripoti yeyote unayo hitaji.
  • 10- Kuna mipaka ya madaraka ya wasimamizi wa program hii.

Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi ya Maahadi ya Wataalamu wa Alkafeel na uendelezaji wa vipaji iliyopo katika mkoa mtukufu wa Karbala, barabara ya Abbasi (a.s) karibu na jengo la mkuu wa mkoa au piga simu zifuatazo: 07711711190/ 07829040001/ 07602323004.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: