Kati ya washiriki (70): Wanawake mahafidhi wa Qur’an tukufu katika kitengo cha Maahadi ya Qur’an wapata nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Qur’an Naeem awamu ya kwanza kipengele cha Tajweed..

Maoni katika picha
Mahafidh wa kike katika Maahadi ya Qur’an chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata nafasi ya kwanza katika mashindano ya Qur’an ya kitaifa upande wa Tajweed, mashindano hayo yameandaliwa na kusimamiwa na idara ya ufundishaji wa Qur’an chini ya ofisi ya Tabligh kitengo cha wanawake katika Atabatu Husseiniyya tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo (Qur’an ni mwenendo wa ushindi wetu), kulikua na washiriki (70) mahafidh na wasomaji wa Qur’an tukufu, kutoka Bagdad, Karbala, Najafu, Baabil, Waasit, Misaan, Basra, Dhiqaar, Muthana, Arbeel, Swalahudin na Diyala.

Hii sio mara ya kwanza kupata ushindi wasomaji wetu, hata katika mashindano ya siku za nyuma walipata nafasi za mwanzo, hii inaonyesha ufanisi na umahiri wa idara ya Maahadi.

Kiongozi wa ufundishaji wa Qur’an tukufu Ustadhat Intiswaar Fadhil alisema kua: “Hakika mashindano hulenga kuonyesha kipawa na uwezo wa msomaji, na husaidia kuwaandaa mahafidh na wasomaji kwa ajili ya mashindano ya kimataifa”.

Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i) alipokea washindi wa mashindano haya katika ofisi yake na akawahusia wasiache kuendeleza vipaji vyao hadi washiriki mashindano ya kimataifa, na mwishoni mwa maongezi yao aliwapa vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: