Atabatu Abbasiyya tukufu yazawadiwa nakala nadra ya Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Muandishi raia wa Iran Sayyid Ali Asghar Mussawiyaan kutoka katika jamhuri ya kiislamu ya Iran, ameizawadia Atabatu Abbasiyya nakala ya Qur’an tukufu yenye maandishi ya aina tau, ambayo ni Thuluth, Nashk na Raihana, aina hizo ni miongoni mwa aina tisa ambazo ni nadra sana, kazi ya kuandika Qur’an hii ilichukua miaka miwili kwa kufanya kazi kila siku masaa kumi.

Bwana Mussawiyaan akasema kua: “Naona fahari kubwa kukabidhi zawadi hii katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) nimatarajio yangu kua itakubaliwa, nakala hii imeandikwa kwa kutumia jiwe la asili lililo chongwa kwa umaridadi wa hali ya juu, hii nakala inauzito wa kilo thelathini, ninatarajia kuandika nakala zingine nakuzitoa zawadi katika Ataba tukufu za Iraq”.

Viongozi wa Ataba walionyesha kuthamini sana juhudi na kazi ya Mussawiyaan ya uandishi wa hii nakala, wakamthibitishia kua malipo yake atayakuta kwa Mwenyezi Mungu, na wakamuambia kua jina lake litaingizwa katika kumbukumbu za Ataba tukufu na litaenziwa milele katika malalo ya mwezi wa bani Hashim (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu ikampa zawadi kama sehemu ya kuonyesha kujali juhudi zake tukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inavitu vingi ilivyo pewa na watu tofauti kutoka ndani na nje ya Iraq, kuna walio toa kama sehemu ya kutekeleza nadhiri zao na wengine kama zawadi tu, kuna utaratibu maalumu wa upokeaji wa vitu hivyo, huandaliwa nakala mbili za waraka wenye jina la mtoaji na kitu anacho toa, moja hupewa mtoaji na nyingine hutunzwa katika sehemu maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: