Atabatu Abbasiyya tukufu yatuma msafara wa misaada kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi mpakani mwa Iraq na Sirya..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea kutuma misaada kwa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi, mara hii wamefunga safari hadi katika mpaka wa Iraq na Sirya waliko majemedari wa Hashdi Sha’abi baada ya kuyatimua magaidi ya Daesh.

Huu ni miongoni mwa misafara mingi inayo tumwa na kamati ya misaada ya Atabatu Abbasiyya tukufu. Kiongozi wa msafara Shekh Haidari Aridhi alisema kua: “Kufuatia maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo taka kuwasaidia wapiganaji wanao pambana na magaidi ya Daesh, pia ukizingatia kua ni sehemu ya wajibu wa Ataba kimaadili na kisheria, Ataba tukufu imetuma msafara huu wa misaada na kuangalia hali za wapiganaji”.

Akaongeza kusema kua: “Tumebeba nafaka mbalimbali za vyakula na kuzigawa kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi waliopo katika mpaka wa Iraq na Sirya, hali kadhalika tulitoa misaada kwa wapiganaji waliopo katika mji wa Sanjaar na Ba’aji, ugawaji wa vyakula hivyo unaenda pamoja na utoaji wa nasaha za kuwajenga kimanawiyya na kuinua ari zaidi, na kuwahusia kuendelea kua na msimamo na subira dhidi ya magaidi ya Daesh. Jambo hilo lilifanywa na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Huu ni miongoni mwa misafara mingi inayo tumwa kwenda kutoa misaada katika vikosi vya wapiganaji waliopa katika uwanja wa vita, hufikishiwa misaada ya moja kwa moja”. Kumbuka kua: “Utumwaji wa misafara hii ulianza siku chache baada ya kutolewa kwa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, na bado tunaendelea hadi itakapo kombolewa ncha ya mwisho ya aridhi ya nchi hii, hakika kila tunacho wapa hawa wapiganaji watukufu ni kidogo sana, kutokana na utukufu mkubwa walio anao kwetu na sisi ni wadaiwa wa kulipa fadhila”.

Shekh Aridhi akasisitiza kua: “Pamoja na mazingira magumu ya hali ya hewa, joto, upepo.. bado kuna watu wamesimama imara kupambana, na msukumo pekee walionao ni uzalendo na kuilinda aridhi hii tukufu”.

Wapiganaji wa Hashdi takatifu walitoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, namna inavyo wajali na kusimama pamoja nao daima katika uwanja wa vita, wakasisitiza kua; kuwajali huko kunawaongezea hamasa na ushujaa wa kuendelea kupambana hadi dakika ya mwisho ya ushindi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutuma misaada mara kwa mara kwa vikosi mbalimbali vya wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, pamoja na kuunda kamati maalumu za kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: