Ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za Abbasi (a.s) za makazi ya watumishi..

Sayyid Swafi
Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amezungumza katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za Abbasi (a.s) za makazi, uliofanyika alasiri ya Juma Nne (8 Dhulqa’adah 1438h sawa na 1 Agosti 2017m) ndani ya jengo la Shekh Kuleiniy lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amesema kua:

“Hakika ndugu zetu watukufu wanao zitumikia Ataba takatifu, na kuchagua kumtumikia Sayyid Shuhadaa (a.s) na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamechagua jambo jema sana hapa duniani kwa kujitolea kufanya kazi katika Ataba hizo takatifu na kuwahudumia mazuwaru watukufu, ikawa ni wajibu kwa uongozi wa Atabatu Abbasiyya ufanye kila uwezalo kwa ajili ya watumishi hawa, ndipo ukaamua kujenga mradi huu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu baada ya miaka mitatu ya kupambana na kuhangaika, hatimae mradi umekamilika; sasa watumishi wetu watukufu watapata nyumba bora za makazi yao na familia zao”.

Akaongeza kua: “Mradi huu una nyumba mia nane za makazi zote zipo tayali kwa makazi, kwa sasa mradi unaanza kutoa huduma kwa watumishi, baada ya hafla hii –Inshaallah- tutaelekea katika nyumba hizo, baadhi ya mida nimekua nikisema na leo narudia kusema mbele yenu; natamani kukamilisha ndoto nyingine, kuna watu wameitumikia Iraq na wakajitolea rohu zao na kumwaga tamu zao takatifu kwa ajili ya nchi iendelee kua na amani na kulinda utukufu wake, jambo hilo limefanikiwa Alhamdu lilaah, watu hawa vipenzi walio mwaga damu zao kwa ajili ya taifa lao, wamefanya jambo kubwa sana kwa nchi yao, hakuna anaye weza kukanusha hili, nawahusia wenye mamlaka; msiziache familia za watu hawa zikaja kuwaomba kitu duni miongoni mwa haki zao za msingi, fanyeni hima kuwatekelezea haki zao kabla hawaja kuombeni, bila shaka anaemiliki nyumba ya kuishi anajihisi utaifa na asie na nyumba hujihisi ugeni, ndugu waliotoa roho zao katika miaka hii hususan baada ya fitna ya Daesh, walipo hisi hatari kwa taifa lao na raia wake, na mara tu baada ya kutamka Marjaa dini mkuu kuhusu nini wanapasa kufanya wakajitokeza wakiwa na furaha kubwa kwa sababu walitambua wanatekeleza wajibu wa dini na taifa lao”.

Akabainisha kua: “Tumetaja zaidi ya mara moja kua katika taifa letu kuna matatizo na utatuzi, amma utatuzi; taifa hili lina uwezo mkubwa na akili pevu zipo nyingi, hivyo taifa linaweza kutatua matatizo mengi.

Tatizo lingine Iraq ni nchi ya kihistoria, lakini hatuandiki historia wala hatutunzi kumbukumbu, tunatoka jasho sana, tu watu muhimu lakini hatutunzi mambo yetu, utunzaji wa mambo hivi leo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa, watu wa Iraq wameendelea kua watukufu kutokana na damu za vijana wao, na leo damu za wairaq zimeturejeshea theluthi ya nchi baada ya kutekwa na magaidi ya Daesh, ndugu hawa na familia zilizo jitolea damu za watoto wao –nazungumza na nina amini wenye mamlaka wanahisi machungu yao- Hakika ndugu hawa wanasubiri kufanyiwa wema zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: