Kitengo cha godaun katika Atabatu Abbasiyya tukufu chahitimisha semina ya (Uandishi wa mazungumzo na ujumbe rasmi wa kiserikali)..

Mtihani wa kumaliza semina
Kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo na kujenga uwezo wa kiofisi ambacho ni miongoni mwa vitengo vya wizara ya mipango ya Iraq, kitengo cha godaun cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimehitimisha semina ya kujenga uwezo kwa watumishi wake iliyo fanyika katika jengo la Ali Haadi (a.s), iliyokua na anuani isemayo: (Uandishi wa mazungumzo na ujumbe rasmi wa kiserikali), semina iliyo lenga kujenga uwezo wa watumishi katika uandishi wa ujumbe na taarifa rasmi pamoja na mazungumzo baina ya vitengo vya Ataba na sekta zingine, semina hii pamoja na zingine nyingi hufanywa kwa lengo la kuongeza uwezo wa watumishi katika nyanja mbalimbali.

Kuhusu semina hii; makamo rais wa kituo cha utafiti cha kitaifa Ustadhi Aadil Arnusi alisema kua: “Semina hii ilihusu mafhum (uwelewa) wa ujumbe na mazungumzo kitaalamu katika maandishi na mazungumzo rasmi baina ya vitengo vya Ataba na idara za kiserikali, na lengo kuu ni namna ya kutambua uongeaji wa mtu na jinsi ya kuandika maelezo yake kwa ufaswaha na kufuata kanuni za lugha ya kiarabu, pamoja na kuwajulisha baadhi ya makosa ya kilugha yanayo fanywa sana na watu wanapo ongea, pia walifanya mazoezi ya vitendo na walipewa mifano hai ya kuandika ujumbe na kuutuma sehemu husika”

Akaongeza kua: “Semina ilidumu siku tano, kila siku ilikua na saa nne za masomo, siku ya mwisho walifanya mitihani, washiriki jumla walikua (20) na wote walipewa vyeti vya ushiriki wa semina hii”.

Tunapenda kukumbusha kua kitengo cha godaun katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu sana, kufanya kazi katika kitengo hiki inahitaji umakini mkubwa kutokana na vitu mbalimbali wanavyo tunza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: