Katika ziara yeke ya kukagua maji mbadala wa mto Furat: Waziri wa maji wa Iraq asisitiza kua Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kazi ya kubadilisha jangwa kame kua sehemu yenye maji na bora kwa kilimo..

Maoni katika picha
Waziri wa maji wa Iraq bwana Hassan Janabi ametembelea Atabatu Abbasiyya na kukagua mradi wa kutumia maji mbadala wa mto Furat unao fanywa na Ataba tukufu.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawaad Hasanawiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu ziara hii kua: “Hakika ziara ya waziri ni sehemu ya kukamilisha ziara yake ya kwanza aliyo kagua miradi muhimu ya Ataba, katika ziara ile alifafanuliwa kuhusu ukubwa wa mradi wa kutumia maji mbadala na faida zake”.

Akaongeza kusema kua: “Kabla ya ziara hii –katika ziara iliyo pita- waziri alikutana na Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na akapewa maelezo kuhusu baadhi ya miradi inayo fanywa na Ataba tukufu ukiwemo mradi wa kutumia maji mbadala, huu ni miongoni mwa miradi muhimu sana kwa mustaqbali wa mji wa Karbala iwapo litatokea tatizo lolote –Allah atuepushie- Muheshimiwa waziri alipata shauku kubwa ya kutembelea mradi huo”.

Waziri wamaji alibainisha kua: “Ataba inapitia katika maendeleo ya kiujenzi na kimazingira, ina mchango mkubwa katika kubadilisha sehemu kame za jangwani kua sehemu zenye maji na kijani kibichi zifaazo kwa kilimo, utukufu wa yote haya uwaendee viongozi wa Ataba chini ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria na kamati kuu ya uongozi pamoja na marais wa vitengo hali kadhalika watumishi wote wa aridhi hii takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: