Tarehe 11 Dhulqa’adah iliangaza nuru ya Imamu Ridha (a.s)..

Maoni katika picha
Tarehe 11 ya mwezi mtukufu wa Dhulqa’adah mwaka (148h) katika mji wa Madina, walimwengu walineemeka kwa kuzaliwa nuru tukufu miongoni mwa nuru za uimamu, nyumba ya Imamu Mussa bun Jafari (a.s) ilijawa na furaha kwa kuzaliwa mtu aliye tukuzwa na Mwenyezi Mungu, mbingu na aridhi vilinawirika kwa kuzaliwa Imamu Ali bun Mussa Ridha, pia anaitwa Murtaza (a.s), alizaliwa baada ya miaka hamsini toka kufariki kwa babu yake imamu Swadiq (a.s), mama yake anaitwa Ummu Walad na jina lake ni (Tuktum) pia inasemekana anaitwa (Najma) alikua ni mwanamke bora kwa akili na dini, Imamu Kadhim (a.s) alikua akimwita kwa sifa ya Twahira (mtakasifu).

Miongoni mwa mambo maarufu kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s), uhai wa maasumu huanza kwa karama na huisha kwa karama, kuhusu imamu Ridha (a.s) anakarama ya siri, ambayo ni karaba ya kabla ya kuzaliwa kwake, imepokewa kutoka kwa Mufidi kutoka kwa Shekh Swaduuq kwa riwaya inayo fika hadi kwa Ali bun Maitham kutoka kwa baba yake, anasema: Nilimsikia Najma mama wa Ridha akisema: “Nilipo pata ujauzito wa mwanangu Ridha sikuhisi uzito wotote, kila nikilala nilikua nasikia tasbihi na tahlili kutoka tumboni mwangu, na nikiamka sisikii kitu, nilipo mzaa aliweka uso wake katika aridhi kisha akainua kichwa chake mbinguni huku mdomo wake unacheza kama mtu anaye ongea, akaingia baba yake Imamu Mussa bun Jafari (a.s) akasema: “Hongera sana ewe Najma, una utukufu mkubwa kutoka kwa Mola wako” nikampa mtoto akiwa katika kitambaa cheupe, akamchukua na kumuadhinia katika sikio la kulia na akamkimia katika sikio la kushoto, akachukua maji ya mto Furat akamuwekea katika taya zake, kisha akamrejesha kwangu na kuniambia: “Mchukue ewe Najma hakika huyu ni Baqiyyatu Llahi katika aridhi”.

Kuzaliwa kwake (a.s) ni kuhuika kwa utukufu na tauhidi, hakika (a.s) alikua ni kiongozi wa kiroho aliye kuja kuwaokoa watu kutoka katika dimbwi la maasi na matamanio, naye ni imamu wa nane miongoni mwa maimamu wa nyumba ya mtume watakasifu (a.s), amebarikiwa siku aliyo zaliwa pia ni baraka kwa watu na tunu ya Mola kwa waja wake, Mwenyezi Mungu atuwezeshe kumtembelea katika dunia, na akhera aturuzuku shifaa yake, na hiyo ni neema ya pekee na kufaulu kukubwa, amani iwe kwake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uawa kwa sumu na siku atakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: