Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa uongozi mkuu wanaendesha mafunzo ya bure kwa wanafunzi mayatima wa mkoa mtukufu wa Karbala wa shule za msingi, kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la sita katika masomo yote, semina hizo zitadumu mwezi mzima kwa mujibu wa ratiba ilivyo pangwa, semina za wavulana zinafanyika katika majengo ya shule ya Saaqi ya wavulana huku semina za wasichana zikiendeshwa katika majengo ya msingi Ameed ya wasichana.
Katika semina hizi wameshiriki makumi ya wanafunzi, wapo walio maliza masomo yao na wale wanao penda kujiendeleza katika masomo, wamewekewa kila kitu kinacho hitajika katika kujifundisha.
Mtu wa habari kutoka katika shule ya msingi ya Saaqi ya wavulana Ustadhat Aayah Zuhair alisema kua: “Shule imepokea wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita wa shule za msingi, katika semina hizi yanafundishwa masomo yote muhimu na kutakua na masomo ya ziada kwa makundi maalumu, mfano masomo ya harakati, maelekezo na sikio sikivu, semina hizi zitafanyika siku nne kwa wiki na kila siku inavipindi sita, hali kadhalika wameandaliwa chakula kila siku, pamoja na usafiri na vifaa vya kusomea”.
Kumbuka kua program hii ni miongoni mwa juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu za kuhakikisha inatoa msaada kwa mayatima katika kila sekta, ili kuwafanya wasihisi unyengo kutokana na uyatima wao.