Mwakilishi wa Vatikan nchini Iraq Albetor Ortigha amesema kua: “Hakika fatwa ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh.w) ya kuilinda Iraq na maeneo matakatifu ndio iliyo okoa Iraq na kulinda umoja wa taifa hili, na kufelisha njama za magaidi ya Daesh, tunafurahishwa sana na maamuzi yanayo chukuliwa, hakika yanakubalika na kila mtu, yameisaidia serikali ya Iraq na kuifanya kua imara, imeweza kuwapiga magaidi na kuwamaliza”.
Haya yalisemwa katika kikao kilicho husisha ujumbe wa Ataba Mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) kufuatia ziara waliyo fanya katika ofisi ya muwakilishi wa Vatikan iliyopo mji mkuu wa Iraq huko Bagdad.
Akaongeza kusema kua: “Nilifurahi sana kupata nafasi ya kushiriki katika kongamano la kitamaduni na kimataira Rabiu Shahada ya kumi na tatu, ninatamani kupata tena nafasi hiyo, pia nilifurahi sana kuona watu wengi muhimu kutoka nchi mbalimbali wanakutana katika aridhi ile takatifu, inapasa sehemu ile iwe ni mahala pakubadilishana mawazo na tamaduni za dini tofauti, ni muhimu sana kuwepo kwa kongamano kama lile na nimuhimu sana likawa endelevu, hususan katika kipindi hiki ambacho Iraq inapita ni muhimu sana jambo hilo, Tumefurahi sana kutokana na ushindi wa jeshi la Iraq, inatakiwa kuwe na ushindi mwingine mkubwa zaidi ya huu ambao ni ushindi wa kifikra”.
Mjume wa ugeni ambaye pia ni makamo rais wa kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Qassim Awaadi alisema kua: “Lengo la ziara yetu ilikua ni kumpa balozi wa Vatikan midani ya kongamano la Rabiu Shahada la mara ya mwisho, alitupokea kwa bashasha kubwa, na tukazungumzia kuhusu ushindi wa jeshi la serikali pamoja na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi ya Daesh, hali kadhalika kuanza kwa hatua ya kupiga vita fikra za kujenga chuki, naye balozi aliashiria alicho kiona katika kongamano la Rabiu Shahada, uhudhuriaji wa watu muhimu kutoka katika nchi mbalimbali duniani, akasema: Nilipata furaha kubwa sana kuwasilishwa ujumbe wa Papa nikiwa katika aridhi takatifu ya Karbala aridhi inayo beba moyo wa Uislamu wa kupendana, nilituma salamu ya kumualika atembelee Karbala takatifu, na nilimfikishia salamu za viongozi wote wa Ataba mbili tukufu, mwisho wa kikao chetu alituaga kwa bashasha kubwa kama alivyo tupokea”.
Mwisho wa kikao ugeni wa Ataba ulimshukuru balozi wa Vatikan na wakamualika azitembelee Ataba tukufu katika mji wa Karbala pamoja na kumpa mwaliko rasmi wa kushiriki katika kongamano la Rabiu Shahada lijalo, pia balozi alionyesha furaha kubwa na akawashukuru sana wageni wake watukufu na akawaombea kudumu katika amani na mapenzi.