Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu apokea bendera ya Atabatu Ridhawiyya tukufu na ataka kuongezeka ushirikiano baina ya pande mbili katika kuwahudumia mazuwaru watukufu..

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa imamu wa nane mtukufu (a.s) katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) amepokea bendera ya kubba ya imamu Ridha (a.s), alipo kua akiupokea ugeni kutoka katika Atabatu Ridhawiyya takatifu walio kuja kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Utoaji wa bendera ni desturi ambayo hufanywa kila mwaka na watumishi wa Atabatu Ridhawiyya tukufu kwa Ataba za Iraq, pamoja na miji mingine kama sehemu ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridha (a.s).

Katika tukio la kupokea bendera yalifanyika mazungumzo baina yao, muhimu zaidi ni yale aliyo sisitiza katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuendelea kushirikiana baina ya Ataba tukufu kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu na kubadilishana uzoefu, pia alitoa shukrani za dhati kwa ugeni huo.

Kumbuka kua tukio hili ni desturi ambayo hufanywa na watumishi wa Atabatu Ridhawiyya kila mwaka, na huu ni mwaka wa nane mfululizo, hutembea na bendera tukufu ya malalo ya imamu Ridha (a.s) ndani ya miji ya Iran katika siku kumi tukufu, zinazo tenganisha baina ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Maasuma na kuzaliwa kwa kaka yake Imamu Ali Ridha (a.s), hutembea na bendera hiyo katika mikoa ya Inan kisha huja nayo katika miji ya Iraq hususan katika Ataba za Karbala na huwatembelea Maraajii na viongozi wa Ataba watukufu huku wakiwa na bendera hiyo takatifu, na mwishoni huitoa zawadi. Pia katika safari hii waliwatembelea majeruhi wa Hashdi Sha’abi waliopo katika hospitali za Najafu na Karbala. Hali kadhalika katika siku hizi hufanyika hafla za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridha (a.s) katika nchi zaidi ya (30) za Ulaya, Asia na Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: