Kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi: Wairaq wanashukuriwa na nchi zote za duniani, kama sio kujitolea kwao muhanga Daesh wangeshambulia kila nchi..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidiy amesema kua, kila nchi inawashukuru wairaq, kama sio kujitolea kwao na kuwasambaratisha Daesh, magaidi hao wangeshambulia kila nchi.

Hayo ameyasema katika kongamano la kusherehekea ushindi lililo fanywa na kikosi hicho asubuhi ya siku ya Juma Mosi na kupewa jina la: (kongamano la fatwa ya ushindi), katika chuo kikuu cha Bagdadi, kama sehemu ya kusherehekea ushindi wa wairaq wa kukomboa mji wa Mosul.

Akaongeza kusema kua: “Nina furaha kubwa kusimama mbele yenu katika kongamano hili tukufu la kusherehekea ushindi wa jeshi letu tukufu na Hashdi Sha’abi pamoja na Hashdi Asha’iri dhidi ya magaidi ya Daesh”.

Zaidiy akataja nukta muhimu zifuatazo:

  • 1- Ushindi huu mtukufu ulio andika historia ya ushujaa na kujitolea kwa wairaq usinge patikana kama sio kutolewa kwa fatwa na Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh).
  • 2- Fatwa ya Marjaa dini mkuu ilikua ndio sababu ya kuto wekwa uhai wetu reheni kwa Daesh.
  • 3- Fatwa ilikua ndio taa la umma na dawa ya gonjwa lililo ikumba nchi yetu tukufu likataka kuitawala na kuisambaratisha, lakini halikuwezekana hilo katika nchi ambayo watu wake wamepata taufiqi ya kuitikia wito wa Marjaa mtukufu.
  • 4- Kila nchi inawashukuru wairaq, kama sio kujitolea kwao muhanga na kuwasambaratisha Daesh, magaidi hao wangeshambulia kila nchi.
  • 5- Tunaiambia kila nchi kua; kutokana na damu za vijana wetu, damu zunu zimesalimika, na kwa juhudi za makomando wetu na subira za kina mama na kina baba wetu mmepata neema ya utulivu na amani, wafundisheni watoto wenu utukufu wa wairaq, na inatakiwa vizazi virithishane taarifa ya wairaq kuwashinda magaidi ya Daesh.
  • 6- Kutokana na fatwa tukufu, ilianzishwa Hashdi takatifu kama zao la pumzi tukufu ya Marjaa dini mkuu.
  • 7- Hashdi Sha’abi wana nafasi muhimu katika ulinzi wa taifa hili na wana mchango mkubwa katika kuwashinda Daesh.
  • 8- Kikosi cha Abbasi (a.s) ni moja ya vikosi vya Hashdi Sha’abi ambao ni nguzo muhimu katika ulinzi wa taifa hili.
  • 9- Tunasisitiza kua sisi ni wasaidizi muhimu wa jeshi letu tukufu, tutaendelea kupokea na kutekeleza maagizo kutoka kwa viongozi wakuu wa jeshi na tutasimama imara kuilinda taifa letu.
  • 10- Tunamshukuru sana mkuu wa majeshi na mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na vikosi vyote vya majeshi bila kuisahau wizara ya ulinzi ambayo imetoa mchango mkubwa sana katika ukisaidia kikosi cha Abbasi kwa hali na mali, pamoja na wizara ya mambo ya ndani ambayo imetupa msaada mkubwa wa mafunzo ya kisheshi, pamoja na kikosi cha kupambana na ugaidi.
  • 11- Tunawashukuru sana viongozi wa Hashdi Sha’abi, watu hawa, wamethibitisha uzalendo wao na kwamba wapo kwa ajili ya kulinda kila raia wa Iraq, aidha tunawashukuru vikundi vya Husseiniyya walio fanya kazi kubwa ya kuwasaidia wanajeshi watukufu, na shukrani za pekee ziwaendee wawakilishi wa Marjaa dini mkuu waliokua pamoja na wapiganaji katika uwanja wa vita wakitoa misaada ya kila aina pamoja na kuwajenga wapiganaji watukufu kiroho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: