Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi: Nakala kale za kiarabu na morosikiyya ni urithi mkubwa wa kihistoria yapasa kuangaziwa..

Maoni katika picha
Kiongozi wa kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi Ustadh Swalaah Mahdi Abdul-wahabi amesema kua; nakala kale zilizoandikwa kwa lugha ya Moroskiyya (kiarabu cha Hispania) zina umuhimu mkubwa, wayapasa watafiti na vituo vinavyo husika na nakala kale kuzipa umuhimu kutokana na ujumbe wa kihistoria zinao beba.

Hayo yamesemwa katika nadwa iliyo endeshwa na kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi chini ya idara ya maktaba katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) iliyo kua na anuani isemayo (Nakala kale za kiarabu na kimoroskiyya katika maktaba za Hispania na Italiya), alitoa muhadhara dokta wa kiiraq aliye bobea katika mambo hayo bwana Muhandi Tamimi, Ustadh Swalaah akaongeza kusema kua: “Hakika Dokta Tamimi alielezea uwepo wa nakala kale kadhaa adimu katika maktaba za Madridi, Dairi Iskariali pamoja na Vatikan, zilizo hifadhiwa katika faharasi na zisizo hifadhiwa, akafafanua kwa kina kuhusu nakala kale hizo na ujumbe zilionao ambao umeandikwa kwa lugha ya Moroskiyya (kiarabu cha Hispania) ambapo yapasa kuziangazia na kuzipa umuhimu unao faa”.

Miongoni mwa walio hudhuria nadwa hii ni Ustadh (Ali Swafaar) ambaye ni msaidizi wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mchango wake alizungumzia umuhimu wa nadwa hii na urithi wa kihistoria wa nakala hizo pamoja na umuhimu wa kuhamisha taarifa hizi kutoka kizazi hadi kizazi kingine, ili kuelezea yaliyo jiri katika historia ya ulimwengu wa kiislamu, katika zama ambazo uislamu ulitawala sehemu kubwa ya dunia, mwishoni Dokta mhadhiri wa nadwa hii alitoa vyeti kwa wasimamizi na waandaaji wa nadwa, kwa ajili ya kuonyesha thamani ya juhudi zao kwa kuandaa nadwa muhimu na yenye athari kubwa kwa washiriki.

Nadwa ilihudhuriwa na watu maalum kutoka katika kituo cha turathi za Karbala na kituo cha uhuishaji wa turathi na maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: