Atabatu Abbasiyya tukufu yatuma shehena ya misaada kwa wakimbizi wa Mosul..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma shehena ya misaada kwa wakimbizi wa Mosul waliopo katika mahema ya (Tal-Ummu Jarabii) katika tarafa ya Tal-Abatwa, wanao kumbana na mazingira magumu kutokana na wingi wao na uchache wa huduma za kibinadamu katika eneo hilo.

Msafara huu wa misaada unasimamiwa na kamati ya maelekezo na misaada, nao ni sehemu tu ya misafara mingi ya misaada inayo tumwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuwasaidia wakimbizi katika sehemu mbalimbali hapa nchini, misaada hii ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Marjaa dini mkuu yanayo himiza kuwasaidia wakimbizi.

Msaada ulihusisha ugawaji wa vikapu vya nafaka za vyakula, pamoja na mabarafu kutoka katika kiwanda cha barafu cha Ataba tukufu, walikua na haja kubwa ya barafu kutokana na joto kali lililopo hivi sasa, pia ugeni unaogawa misaada ulitembelea hema za wakimbizi na kusikiliza matatizo yao, hakika wana matatizo makubwa, inatakiwa serikali na taasisi za kibinadamu kuongeza juhudi katika kuwasaidia, misaada tunayo wapa haitoshi kumaliza shida zao hata kidogo.

Kwa upande wao (wakimbizi), walishukuru sana juhudi zinazo fanywa na Marjaa dini mkuu pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu, za upendo huu wa mzazi kwa wanae, katika kuwalea na kuwasaidia wakimbizi na kuwatembelea kila wakati pamoja na kutoa misaada mfululizo katika mazingira magumu kama haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: