Kituo cha uchapishaji wa vitabu cha Alkafeel kimekua cha kwanza kukamilisha kazi za wizara ya malezi na chathibitisha uwezo wa kuchapa zaidi..

Maoni katika picha
Mkuu wa Darul Kafeel inayo husika na uchapaji pamoja na usambazaji wa vitabu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Faras Ibrahimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kituo cha uchapaji kimemaliza kazi yote kiliyo pewa na wizara ya malezi ya kuchapa vitabu vya masomo ndani ya muda walio kubaliana, tena kabla ya muda huo kuisha, kimekua kituo cha kwanza kupewa kazi na wizara ya kuchapisha vitavu vya maosomo na kuimaliza kwa muda uliopangwa tena katika ubora mkubwa, kuanzia majarada, karatasi wino na vinginevyo ambavyo vimefanya nakala hizo kua bora zaidi”.

Akaongeza kusema kua: “Kutokana na mkataba walio ingia kituo cha uchapaji na wizara, wamekabidhi nakala (2,658,000) za aina tasi na viwango tofauti, makabidhiano hayo yamehudhuriwa na kamati maalumu kutoka wizara ya malezi ya Iraq, ambao walitembelea mara kwa mara kituo cha uchapaji wakati wa uchapaji wa vitabu hivyo, wote kwa ujumla wamesifu ubora wa vitabu na wameahidi kuongeza ushirikiano kwa maslahi ya pande zote mbili, na manufaa ya elimu na malezi ya wairaq”.

Ibrahimi akasisitiza kua: “Hakika kituo cha uchapaji, kutokana na zana kilizo nazo pamoja na wataalamu wake wenye uzoefu mkubwa wanao uwezo wa kuchapa vitabu vingi zaidi ya idadi hii”.

Akasema kua: “Tumezingatia mambo mengi katika uchapaji wa vitabu hivi vya masomo, miongoni mwa mabo hayo ni:

  • 1- Aina ya karatasi, karatasi hizi zimetengenezwa Ulaya; ni rafiki wa mazingira na zinashikika vizuri.
  • 2- Rangi tulizo tumia zina muonekano mzuri sana.
  • 3- Majarada ya vitabu yamewekwa kwa utaalamu mkubwa yanamuwezesha mwanafunzi kufungua kurasa za kitabu kwa urahisi bila kuharibu karatasi.
  • 4- Muonekano mzuri wa maandishi na picha, na hili linatokana na ubora wa mashine ya kuchapa, ambayo ni mashine ya kisasa yenyo ubora mkubwa.
  • 5- Njia ya kugandisha na kubana karatasi, kila kitabu kumebanywa vizuri kutokana na ukubwa pamoja na idadi ya karatasi zake.
  • 6- Wino wa maandishi ni mzuri unao endana na aina za karatasi.
  • 7- Kituo cha uchapaji ni cha wairaq na kinaendeshwa na wairaq, hivyo tunachangia sera ya kujitegemea kama taifa na sio kutegemea vituo vya nje.

Kumbuka kua miongoni mwa sababu muhimu zilizo ifanya wizara ya malezi kuchapisha vitabu vyake katika kituo cha Alkafeel, ni ufanisi walio onyesha na kituo hiki katika kazi zao, ulio sifiwa na taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi, hakika machapisho yake yote yanakidhi vigezo vya kimataifa na yanafikia viwango vilivyo wekwa na taasisi ya kudhibiti ubora ya Iraq, aidha yanashindana na machapisho ya vituo vikubwa vya kimataifa na kuyashinda machapisho mengi ya kitaifa kwa mujubu wa shuhuda za wataalamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: