Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chaanza upanuzu wa maegesho maalimu ya magari ya Atabatu Abbasiyya na chaongeza idadi ya vyoo..

Maoni katika picha
Miongeni mwa mipango yake ya maendeleo, na kuandaa maeneo yanayo hitajika kutumiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya ndani na nje, kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Ataba, kimeanza upanuzi wa maegesho ya magari ya Shahid (Maahir) kwa ajili ya kuegeshea magari ya Atabatu Abbasiyya tukufu, maegesho hayo ni muhimu sana, yapo katika barabara ya Hauli inayo unganisha baina ya Karbala na Najafu.

Muhandisi Swafaa Muhammad Ali kutoka kitengo cha usimamizi wa kihandisi na msimami mkuu wa mradi huu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi huu ni miongoni mwa miradi mingi inayo simamiwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi, hapo awali maegesho haya yalikua hayakidhi haja, baada ya jupewa jukumu la kupanua maegesho haya, tulianza kuandaa michoro na ilipo pasishwa tumeanza ujenzi kama michoro inavyo elekeza”.

Akaongeza kusema kua: “Tumeanza na kumwaga zege la chini litakalo himili uzito wa magari (mitambo) itakayo egeshwa hapa, pamoja na kujenga sehemu maalumu ya kuoshea magari, kama pia tunavyo jenga sehemu za kukaa wahudumu, sehemu ya utawala na sehemu ya vyoo, baada ya kukamilika ujenzi huu kituo hiki kitakabidhiwa katika kitengo cha mitambo (magari) ambao ndio wanufaika wakuu wa mradi huu”.

Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu zaidi, kina idara nyingi na wataalamu wa aina mbalimbali wanaofanya kazi usiku na mchana katika vitengo tofauti vya Ataba tukufu, kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: