Kitengo cha miradi ya kihandisi chaanza kugawa funguo za nyumba za Abbasi za makazi..

Maoni katika picha
Baada ya kukamilika matengenezo ya nyumba za Abbasi (a.s) ambazo zimejengwa kwa ajili ya makazi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzinduliwa wiki iliyo pita, kitengo cha miradi ya kihandisi kimeanza kugawa funguo za nyumba hizo zipatazo (831) kwa kufuata utaratibu ulio wekwa na kitengo hicho katika ugawaji wa nyumba kwa wanufaika.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh na msimamizi mkuu wa ugawaji wa nyumba hizo amesema kua: “Katika wiki hii tumeanza kugawa funguo za nyumba za makazi za Abbasi (a.s) kwa wanufaika, kila siku tunagawa kwa watumishi (50), baada ya kukabidhiwa funguo anaruhusiwa kuhamia katika nyumba yake au kukagua na kama ataona dosari yeyote anatuambia na sisi tunaijulisha kampuni iliyo jenga kwa ajili ya kuja kurekebisha kama mkataba wetu unavyo sema”.

Akaongeza kusema kua: “Kampuni iliyo jenga nyumba hizi ipo tayari kufanya marekebisho yeyote yatakayo hitajika tena kwa haraka iwezekanavyo, ukizingatia kua mradi huu umetekelezwa kwa awamu na nyumba zingine zimejengwa siku nyingi hivyo inawezekana kabisa kukajitokeza dosari ndogo ndogo”.

Akasisitiza kua: “Sisi tunafuata ahadi yetu tuliyo weka, kua tutakabidhi nyumba isiyo kua na dosari na inayo kidhi vigezo vya kiufundi tulivyo weka”.

Tunapenda kukumbusha kua, nyumba za Abbasi (a.s) za makazi ni mradi wa kwanza mkubwa katika mkoa wa Karbala ulio jengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (305000) kiasi cha nyumba za ghorofa (831) pamoja na nyumba za chini, barabara, nyumba za wahudumu, kituo cha afya, shule na sehemu za kupumzika, mradi huu umejengwa katika sehemu ya katikati ya Najafu na Baabil, kwenye makutano ya barabara ya Karbala – Baabil na Karbala – Najafu.

Kumbuka kua lengo la mradi huu ni kuonyesha thamani ya juhudi zinazo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), na kwa ajili ya kuhakikisha watumishi hawa watukufu wanapata makazi bora yanayo endana na maendeleo ya dunia ya leo, watapewa nyumba hizo kwa bei ndogo yenye msaada ndani yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: