Idara ya umwagiliaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu yajitolea kugawa maji kwa mahujaji na kuinua kauli mbiu ya isemayo kunywesheleza mahujaji ni utukufu wetu..

Maoni katika picha
Huduma zinazo tolewa na idara ya umwagiliaji chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu haijaishia kwenye kugawa maji kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) peke yake, bali wanashughuli zingine nyingi wanazo fanya, miongoni mwa shughuli huzo –kwa mwaka wa tatu mfululizo sasa- ni kugawa maji baridi ya kunywa kwa watu wanao kwenda kutekeleza ibada tukufu ya Hija, na wanaopita njia ya nchi kavu (barabara), wanainua kauli mbiu isemayo (kuwatumikia na kuwapa maji ya kunywa mahujaji ni utukufu wetu).

Kiongozi wa idara ya umwagiliaji, Haji Ahmad Hanun ambaye alikuwepo mwenyewe katika kituo cha kupokea misafara ya mahujaji kwenye eneo la mpakani alisema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu ni sehemu ya wajibu wake kuwakirimu wageni wa Mwenyezi Mungu mtukufu, kupitia idara ya umwagiliaji chini ya kitengo cha utumishi, imeandaa maelfu ya lita za maji na vipande vya barafu kwa ajili ya kugawa maji safi na baridi kwa misafara ya mahujaji, na tumeanza kazi hii toka msafara wa kwanza ulio pita (06 Agosti 2017m), na watumishi wanashindana kutuo huduma hii, na itaendelea hadi msafara wa mwisho”.

Akaondeza kusema kua: “Tumejipanga kugawa maji baridi ya kunywa kiasi cha lita (3000) kila siku, kutokana na wingi wa misafara ya mahujaji, tunaweza kuongeza hadi kata -lita- (30000) kwa siku, tumeandaa vituo (60) katika eneo lote la mpaka, tunasambaza maji katika vituo hivyo kwa kutumia magari maalumu, hali kadhalika tumeandaa gari maalumu kwa ajili ya kuhifadhia barafu, linaweza kubeba vipande (600) vya barafu kutoka katika kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasisitiza bwana Hanun kua: “Hakika kutoa huduma hii ni fahari kwetu, kunaongeza utukufu wetu wa kuwatumikia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ambaye alikua mnyweshelezaji wa maji, hakika sisi tunanywesheleza mahujaji kwa jina lake na utukufu wake na baraka zote zimuendee yeye ni sawa na tunanyoosha mikono wake katika kunywesheleza mahujaji”.

Mahujaji walishukuru sana huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwao, na ulinzi mkubwa wanao pewa njiani wanapo tumia barabara kwenda kutekeleza ibada tukufu ya Hijja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: