Muhimu: Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chatoa maelekezo kwa wapiganaji wake na kuhusu kuukomboa mji wa Tal-afar..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetoa maelezo kuhusu wajibu wao baada ya kupokea maswali mengi katika anuani yao rasmi. Fahamu: Anuani za kikosi cha Abbasi (a.s) zimepigwa picha na kuwekwa chini ya habari.

Ifuatayo ni nakala ya maelekezo:

Kufuatia wingi wa maswali yanayo elekezwa kwetu kupitia anuani zetu rasmi, tunatoa maelekezo haya tukitarajia watu wote mtayaona:

  • 1- Tunasikitika kujitolea kumesimamishwa kwa sasa, hakuna taarifa mpya kutoka kwa wakuu wa Hashdi Sha’abi au mishahara hadi itakapo patikana taarifa nyingine.
  • 2- Wanaopenda kushiriki zam kwa kujitolea bila malipo kwa wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) ambao ni wapiganaji wa hakiba pamoja na ndugu zao watumishi wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hasa katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu au katika matukio ya kitaifa, au kushirikiana na wapiganaji katika uwanja wa vita, wanaweza kuwasiliana na viongozi wa maeneo husika kupitia anuani zilizopigwa picha hapo chini.
  • 3- Ndugu mujahidina na watumishi wote:
  • A- Ofisi itachukua taarifa muhimu kwa kila mtumishi kutokana na kikosi pamoja na kitengo chake.
  • B- Maoni na malalamiko yawasilishwe kwa moja ya njia mbili: njia ya kwanza: Sanduku la maoni. Na njia ya pili: Kukutana moja kwa moja na mkuu wa kikosi au msaidizi wake kila siku ya Juma Tatu kuanzia saa (04:00 asubuhi hadi saa 06:00 mchana) na saa (08:00 mchana hadi saa 10:00 jioni) anapokea maoni na malalamoko ya aina zote.
  • C- Familia za mashahidi (M/M awarehemu) na majeruhi wanapewa umuhimu zaidi na wanashughulikiwa kwa namna maalumu.
  • 4- Maelezo kuhusu vita ya kukomboa mji wa Tal-afar Inshallah:

Mawasiliano yatafanyika na wawakilishi wa kikosi katika mikoa, na watashiriki wapiganaji elfu 3 kutoka katika wapiganaji wetu wa hakiba, walio pata mafunzo ya kijeshi yaliyo tolewa na kikosi cha Abbasi (a.s) katika mikoa yote baada ya fatwa ya Marjaa dini mkuu kuhusu umuhimu wa kuwaandaa vijana kivita. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape taufiq ya ushindi wa haraka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: