Kama kawaida katika kila usiku wa Jumaa, Atabatu Abbasiyya tukufu hufungua milango yake kuwapokea maelfu ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umefurika mazuwaru hao watukufu, pamoja na mazingira magumu ya hali ya hewa, na kuongezeka kwa joto havija sababisha kupungua idadi ya watu ambao huja katika eneo hili takatifu.
Wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiongozwa na imani kubwa waliyo nayo pamoja na mipango mizuri iliyo pangwa kila siku ya Ijumaa na katika siku za kawaida, wanafanya kazi kubwa ya kuwatumikia mazuwaru watukufu na kuwarahisishia utekelezaji wa ziara yao pamoja na ufanyaji wa ibada mbalimbali katika mazingira bora zaidi.
Jicho la mtandao wa Alkafeel lilishuhudia kufurika kwa mazuwaru hao na linakuletea picha hizi..