Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya: Kawashukuru wapiganaji watukufu wa vikosi vyote ambao bila wao tusingepata neema ya amani..

Katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (a.t) azungumza katika hafla ya kufunga masomo ya Qur’an ya msimu wa kiangazi yaliyo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, na alielekeza shukrani zake kwa wapiganaji wa vikosi vyote hususan wale wanaojitolea katika kutekeleza fatwa tukufu ya kujilinda na mashahidi pamoja na familia zao, kutokana na nafasi kubwa waliyo nayo katika taifa, raia na maeneo matukufu ya Iraq, kama sio kujitolea kwao muhanga tusinge fanya hafla hii.

Hafla ilifanyika baada ya Aduhuri ya siku ya Ijumaa 18 Dhulqa’adah 1438h sawa na 11 Agosti 2017m katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ifuatayo ni nakala ya khutuba yake:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Rehema na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad na Aali zake watoharifu… Iwe kwenu amani ya Mwenyezi Mungu na baraka zake.

Amesema mtume (s.a.w.w):

(Mimi nakuachieni vizito viwili mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu milele, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha watu wa nyumbani kwangu).

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye tujaalia kua miongoni mwa wanaoshikamana na hadithi ya mtume (s.a.w.w), hususana katika utendaji wa ibada hii ambayo wanafunzi hukaa misikitini na katika husseiniyya na Ataba tukufu wakifundishana Qur’an na kuhifadhishana, jambo hilo ni kuitekeleza kwa vitendo hadithi tukufu ya mtume (s.a.w.w).

Katika mnasaba huu tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye tupa neema kubwa ya kuifanyia kazi Qur’an tukufu, na kutufanya kua katika umma bora wa Mtume (s.a.w.w) na ametujalia kua majirani wa malalo ya maimamu wa nyumba ya mtume, tena katupa utukufu wa kutufanya kua watumishi wa maeneo hayo matakatifu na kuwahudumia mazuwaru wa maeneo hayo, tunamuomba Mwenyezi Mungu azikubali ibada zetu na ibada za wote mliopo hapa, katika sehemu hizi hushuka malaika kila dakika na katika kila sekunde malaika hushuka na kupanda huku tukisomeshana Qur’an.

Mtume (s.a.w.w) anasema: (Mbora wenu ni yule atakaye jifundisha Qur’an na akaifundisha), miongoni mwa utukufu zaidi wa kushukuru neema hii; mwaka wa kwanza tulikua na wanafunzi (150) kisha idadi imeendelea kuongezeka kila mwaka, mwaka ulio fuata wakawa (1500) kisha wakawa (3000) kisha (6000) hadi sasa tuna wanafunzi (16000) kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Pia tunazishukuru familia tukufu zilizo shajihisha watoto wao kuhudhuria masomo haya katika kipindi cha likizo za kiangazi (majira ya joto) ili wanufaike na muda huo kwa kujifunza kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukihifadhi.

Hali kadhalika tunawashukuru wanafunzi watukufu kwa kuvumilia kwenu mazingira magumu ya joto.

Na shukrani za pekee zimuendee kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) mlezi na mdhamini wa kwanza wa harakati hii tukufu bila kuwasahau walimu waliojitolea kufundisha katika semina hii.

Na tunatoa shukrani kwa idara ya Maahadi ya Qur’an tukufu na watumishi wake kwa juhudi kubwa waliyo onyesha pamoja na vitengo vyote vilivyo wasaidia kwa namna moja au nyingine, kama vile kitengo cha mitambo (magari), kitengo cha mgahawa (mudhifu), kitengo cha utumishi, kitengo cha nidham, kitengo cha usimamizi wa haram tukufu, na kila aliye changia kufanikisha mradi huu, bila kuwasahau wapiganaji watukufu wa vikosi vyote hususan wale wanao jitolea na mashahidi wetu wema pamoja na familia zao tukufu, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wetu watukufu na awaponye haraka majeruhi wetu..

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu pamoja na rehema zake na baraka zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: