Idara ya kinga chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeendesha zoezi la kuua wadudu na kutibu mimea kwa kutumia zana mbalimbali, zoezi hili linalenga kutokomeza wadudu wenye madhara kwa binadamu katika vitengo vyote vya Ataba na maeneo wanayo penda kupumzika mazuwaru pamoja na katika hospitali ya Alkafeel.
Kiongozi wa idara ya kinga chini ya kitengo cha utumishi Ustadh Haamid Hussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu kazi hii kua: “Kama mnavyo tambua wadudu wenye madhara kwa binadamu kuna wakati huwa wengi, na hasa wakati wa kiangazi, hivyo kitengo cha kinga kinaendesha zoezi kubwa la kupambana na wadudu hao katika vitengo vyote vya Ataba tukufu vya ndani na nje kwa ajili ya kulinda usalama wa watu na mali kwa kutumia zana mbalimbali, kazi hii imegawanywa katika makundi tofauti, kuna kundi la kupambana na wadudu watambaao aridhini, kundi linalo pambana na wadudu warukao na kundi linalo pambana na maradhi ya mimea”.
Kumbuka kua idara ya kinga chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya kazi kubwa ya kupambana na wadudu warukao na watambaao kwa kutumia zana mbalimbali kwa lengo la kuwatokomeza na kuzuia usambaaji wa wadudu hao.