Mwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika nchi za Ulaya Mheshimiwa Sayyid Murtadha Kashmiri amepongeza mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika nyanja ya majengo na elimu, pia amesifu harakati za kiqur’an zinazo fanywa na Ataba hiyo ndani na nje ya Iraq, kinacho fanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu katika mji mkuu wa Uingereza Landan ni ushahidi wa wazi wa utendaji bora unaofuata misingi ya Qur’an tukufu.
Aliyasema hayo katika hafla ya kufunga semina ya masomo ya Qur’an iliyo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Landan, iliyo fanyika jioni ya siku ya Ijumaa (18 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (11 Agosti 2017m) katika taasisi ya Imamu Khui (q.s), akaongeza kusema kua: “Hakika viongozi wa Maahadi ya Qur’an tukufu wanafanya juhudi kubwa sana wanastahiki pongezi, wanafuata mwenendo bora na madhubuti ambao ni mwenendo wa Qur’an tukufu na kizazi cha mtume kitoharifu, amebarikiwa kila atakae shikamana na lulu hizi tukufu, nawasisitiza wazazi wawahimize watoto wao kuja kushiriki katika semina hizi za Qur’an tukufu”.
Naye mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Dhiyaau-dini Almajidi Zubaidiy mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapicha alipata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo, alitoa shukrani kwa wasimamizi wa semina, akaelezea mambo muhimu yanayo fanywa na tawi la Maahadi ya Qur’an katika mji wa Landan au katika miji mingine, namna wanavyo endesha semina mbalimbali na nadwa kuhusu Qur’an na mengineyo, pia akaelezea mafanikio mbalimbali yaliyo patikana katika Atabatu Abbasiyya tukufu hususan yanayo husiana na Qur’an, kwa kufundisha maelfu ya wanafunzi katika semina za Qur’an tukufu, zinazo endeshwa na Maahadi ya Qur’an pamoja na matawi yake yote, likiwemo tawi la Landan ambalo limesha toa wahitimu karibu (150) wakiume na wakike, walio fundishwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kuamiliana na riwaya za Ahlulbait (a.s), hukumu za usomaji wa Qur’an, Tajwidi na Hifdhu, zilizo fanyika katika miji ya Glasgow, Scotland, Brigham, Livapul na Landan”.
Hafla ikahitimishwa kwa mashairi ya kumsifu mtume (s.a.w.w) na kugawa vyeti kwa washiriki wa semina pamoja na kupandisha bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyo letwa kutoka Karbala kama sehemu ya kutabaruku nayo wahudhuriaji walio kuwepo.