Katika wiki moja, kamati ya misaada chini ya ofisi ya Sayyid Sistani yatuma shehena mbili za misaada kwa watu wa Mosul..

Maoni katika picha
Bado kamati ya misaada chini ya Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) inawasaidia wakimbizi wa Mosul kwa aina mbalimbali za vyakula, kutokana na ratiba yake ya kutoa tani na tani za vyakula kwa ajili ya kuchangia kupunguza mazingira magumu wanayo kumbana nayo hivi sasa, kutokana na maelekezo ya ofisi tukufu ya Marjaa dini mkuu ndani ya wiki moja zimetumwa shehena mbili za misaada, pamoja na mazingira magumu ya hali ya hewa na kiusalama lakini wameweza kufanya kazi kwa mujibu wa ratiba yao.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kamati hiyo Sayyid Shaheed Mussawiy amesema kua:

Shehena ya kwanza ilipelekwa katika mahema ya (Judaa) namba tano yaliyopo kusini ya kitongoji cha Qayaarah katika mkoa wa Nainawa, katika mahema hayo viligawiwa vikapu elfu tano, kila kikapu kilikua na aina nane za nafaka.

Shehena ya pili ilipelekwa katika kijiji cha Imamu Gharbi kilichopo kusini mwa kijiji cha Qayaarah katika mkoa wa Nainawa, ambacho watu wake walikimbia kwa mara ya pili baada ya kushambuliwa na magaidi ya Daesh mwezi mmoja uliopita, wakafanya ufisadi mkubwa, waliua na kuteka baadhi ya wana kijiji, baada ya jeshi la serikali kufanikisha kuwatimua na kukomboa kijiji hicho, wana kijiji waliomba wasaidiwe, ndipo ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh), akaelekeza kamati ya misaada iwapelekee misaada ya chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu, wamepewa vikapu (1600) vya nafaka pia wamepewa na vitu vingine kutokana na mahitaji yao.

Kuhusu radi amali ya wakimbizi Mussawiy alisema kua: “Walikua na radi amali chanya, iliyo jaa shukrani kwa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) kutokana na misaada anayo wapa na kuitikia wito wao, fahamu kua hii ni shehena ya nne ya misaada kwa watu wa kijiji cha Imamu Gharbi toka kuanza kwa vita ya kukomboa mji wa Mosul, miongoni mwa mambo waliyo tuagiza ni: (Tufikishieni salamu zetu kwa Mheshimiwa Sayyid Sistani na wajumbe wa ofisi yake pamoja na kila anaeshiriki katika misaada hii ya kibinadamu bila kuisahau taasisi ya Ain na watumishi wake, waambieni tunawashukuru sana kwa misaada hii, hatujapata misaada mingi kiasi hiki sehemu yeyote zaidi yao, hakika malipo yao watayakuta kwa Mwenyezi Mungu katika mizani ya mema yao); haya yalisemwa na wakimbizi wa mahema ya Judaa, watu wa kijiji cha Imamu Gharbi maneno yao hayakutofautiana na watu wa kijiji cha Qayaarah, mmoja wa wanakijiji alisema kua: (Hakika Sayyid Sistani ametufanya kua wamoja kutokana na misaada yake ya kibinadamu) mwingine akasema kua: (Mimi ni sunni na ninakiri kua Sayyid Sistani ndio Marjaa wangu na hakika ni Marjaa wa wairaq wote) wakaomba wafikishiwe salamu na dua zao za kumuombea umri mrefu na aendelee kua kimbilio la wairaq wote.

Kumbuka kua shehena za misada zinazo tumwa na kamati hii bado zinaendelea chini ya ratiba maalumu katika hema za wakimbizi na miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kuwapunguzia machungu yanayo wakumba na kuwafanya wahisi kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wairaq wote, na kuondoa picha mbaya inayo sambazwa na maadui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: