Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kupitia mkuu wake Ustadh Maitham Zaidiy chatangaza siraha yake mpya itakayo tumika kwa mara ya kwanza katika vita ya Tal-afar iliyo pewa jina la (Muayyad) kama sehemu ya kumuenzi jemedari wake Sayyid Muayyad Hajaar aliye pata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Bashir.
Haya yalisemwa katika mkutano na vyombo vya habari ulio fanyika asubuhi ya leo Juma Tatu (21 Dhulqa’adah 1438h) wasa na (14 Agosti 2017m) baada ya kufanyiwa majaribio kwa siraha hiyo pamoja na siraha nyingine iitwayo (Shihaab).
Zaidiy akabainisha kua, siraha ya Muayyad ni siraha ya kisasa yenye uwezo wa kubaini na kunasa matukio kwa kiwango cha juu, inauwezo wa kuonyesha matukio na picha kwa uwazi, na inaweza kulenga shabaha na kushambulia kwa wakati stahili. Na hiyo siraha nyingine inauwezo wa kuangalia na kushambulia kwa wakati mmoja, utamuona adui kupitia kamera yenye ubora mkubwa na unaweza kuseti utakavyo na itakuonyesha taarifa za adui, imeonganishwa na bunduki inayo weza kufanya kazi moja kwa moja bila kushikwa na mtu, ubunifu huu umefanywa na makamanda wa kikosi cha Abbasi (a.s) na ulikua ni mradi wa kumaliza masomo kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Karbala.
Zaidiy akasisitiza kua: “Hakika siraha hizi zimebuniwa na kuundwa na wairaq halisi na zitatumika kwa mara ya kwanza katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar”. Akaongeza kusema kua: “Leo tumezifanyia majaribio siraha hizi mbili na zote zimethibitisha uwezo wake, siraha hizi zinaingizwa katika orodha ya mafanikio ya kisiraha kama ilivyo ingizwa siraha ya Raqiib yenye uwezo wa kumuona adui kwa umbali wa kilo meta 14 au zaidi”.