Sayyid Swafi autaka uongozi wa shirika la ndege uwajibike kutokana na kuchelewa kwa baadi ya safari zake..

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) siku ya Juma tatu ya (21 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (14 Agosti 2017m) ameutaka uongozi wa shirika la ndege la Iraq uwajibike kutokana na kuchelewesha wasafiri wake katika baadhi za safari.

Katika ujumbe ulionaswa na mtandao wa Alkafeel wa kimataifa Sayyid Swafi (d.i) amesema kua: “Ni wajibu wa viongozi wa shirika la ndege la Iraq kuwajibika kutokana na kuchelewa kwa mara kwa mara kwa safari za ndege zake”.

Aliyasema hayo katika moja ya viwanja vya ndege vya Iraq, kilicho shuhudia kuahirishwa kwa safari ya ndege, jambo hili lina ashiria kurudi nyuma kimaendeleo kwa shirika kongwe la usariri wa anga katika mashariki ya kati na ulimwengu wa kiarabu.

Kumbuka kua shirika la ndege la Iraq, ndio shirika kubwa zaidi la ndege hapa Iraq na ni mwanachama wa usafiri wa anga katika umoja wa nchi za kiarabu, lilianzishwa mwaka wa 1945m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: