Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidiy katika mkutano na vyombo vya habari ulio fanywa asubuhi ya siku ya Juma Tatu (21 Dhulqa’adh 1438h) sawa na (14 Agosti 2017m) alitangaza kua vikosi vitakavyo shiriki katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar ni pamoja na:
Vikosi vinavyo fungamana na Hashdi Sha’abi chini ya kanuni namba (26).
Vikosi vinavyo fungamana na wizara ya ulinzi ya Iraq.
Vikosi vya hakiba miongini mwa vikosi vya Abbasi (a.s), ambao wameitwa kupitia wawakilishi wetu katika kila mkoa, wale walio fundishwa mbinu mbalimbali za kivita.
Tunapenda kukumbusha kua kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya mazoezi ya kivita kwa kutumia siraha nzito nzito za kivita ikiwa ni pamoja na siraha zilizo tengenezwa na wahandisi wa kikosi hicho, na zikathibitisha uwezo wake wa kushambulia na kufikia malengo, pamoja na kufanyia majaribio siraha mpya zitakazo tumika kwa mara ya kwanza katika vita hii..